Wednesday 24th, April 2024
@Uwanja wa Ilulu - Manispaa ya Lindi
Mkoa wa Lindi ndio uliochaguliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019, ambayo yatafanyika katika Uwanja wa Ululu - Manispaa ya Lindi tarehe 14 Octoba, 2019. Maadhimisho haya yanakwenda sambamba na Kumbukizi ya taifa la Tanzania bila hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye anatimiza miaka 20 toka afariki. Aidha, kutakuwa na maadhimisho ya wiki ya vijana ambayo hutoa fursa kwa vijana wa Tanzania zima kuja kuonyesha kazi zao za shughuli za ujasiriamali wanazofanya.
Uongozi wa Mkoa wa Lindi, chini ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Godfrey Zambi unawaalika wadau wote kuja kushiriki katika kilele hicho ikiwa ni pamoja na kushirikiana na mkoa wakati wa maandalizi ya tukio hili muhimu katika taifa letu.
Karibuni sana.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.