Friday 29th, March 2024
@SEA VIEW BEACH RESORT
Mkoa wa Lindi kwa kushirikiana na kampuni ya magazeti ya serikali “Tanzania Standard Newspapers” (TSN) utaendesha kongamano la jukwaa la fursa za biashara na uwekezaji, litakalofanyika ukumbi wa hotel ya SEA VIEW BEACH RESORT iliyopo Lindi mjini. Madhumuni ya kongamano hilo ni kutoa fursa kwa wadau wa Maendeleo, ambao wangependa kufanya biashara na kuwekeza ndani ya mkoa wetu.
Mkoa unazo fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji, katika maeneo ya Kilimo, Madini, Gas, Viwanda, Mifugo, Uvuvi, Utalii, Misitu na ujenzi wa hotels. Fursa hizi bado hazijatumika kikamilifu kuinua uchumi wa wananchi wa Lindi na Watanzania kwa ujumla.
Kufanyika kwa kongamano hili kutaleta chachu kubwa katika kutangaza mkoa na maeneo yenye vivutio vya biashara na uwekezaji. Huko nyuma kulikuwa na changamoto kubwa ya miundombinu na hivyo kuwa sababu ya wafanyabiashara na wawekezaji wengi kusita. Hata hivyo, jitihada kubwa iliyofanywa na serikali, kwa sasa miundombinu ndani ya mkoa imeboreshwa kwa kiwango kikubwa sana, hivyo kutokuwa changamoto tena.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.