Friday 26th, April 2024
@Viwanja vya Ngongo - Manispaa ya Lindi
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius Byakanwa wanawajulisha watanzania wote kuwa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini kwa mwaka 2019 yatafanyika katika Viwanja vya Ngongo – Manispaa ya Lindi.
Hivyo Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi, Wafanyabiashara na wadau mbalimbali mnaalikwa kuja kushiriki kwa kuanzia kipindi hiki cha maandalizi. Maonesho haya yanatoa fursa kubwa katika kuelezea shughuli mnazozifanya, kutoa elimu kwa wakulima na wananchi kwa ujumla kuhusu mambo mbalimbali hasa katika uzalishaji bora, uongezaji thamani wa mazao, masoko na masuala mengine mengi.
Kauli Mbiu ya Maonesho ya Nanenane mwaka 2019 ni "Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Nchi".
Washiriki wote wawasilishe michango yao kupitia Bank of Tanzania, Akaunti Na. 9921169736 yenye jina: SUB TREASURER MISCELLANEOUS EXPENDITURE DEPOSIT ACCOUNT.
Karibuni Sana
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.