• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Huduma ya Maji


TAARIFA YA HALI YA HUDUMA YA MAJI MKOANI LINDI

1.0 Utangulizi

1.1 Hali ya huduma ya Maji Mkoa wa Lindi

Sensa ya mwaka 2012 inaonesha kuwa Mkoa wa Lindi ulikuwa na wakazi wapatao 864,652, hadi kufikia mwezi Agosti, 2018 inakadiriwa jumla ya wakazi 413,503 sawa na asilimia 54.9 ya wakazi waishio vijijini wanapata huduma ya maji safi na salama. Huduma hii inatolewa kwa kutumia vyanzo vya maji vikiwemo visima virefu na visima vifupi vyenye pampu za mkono, miradi ya mtandao wa bomba wa kusukuma kwa mashine, miradi ya maporomoko na uvunaji wa maji ya mvua.

1.1.1  Mpango wa Kuongeza Upatikanaji wa Huduma ya Maji Vijijini

1.1.2  Utekelezaji wa Miradi katika Vijiji 10 katika kila Halmashauri

Hadi kufikia mwezi Agosti, 2018 jumla ya miradi 39  katika Halmashauri za Mkoa wa Lindi inatekelezwa kupitia Mpango wa maendeleo sekta ya maji awamu ya I (WSDP I) ambapo, Halmashauri ya kilwa imetekeleza jumla ya miradi 7 ambayo imekamilika na inahudumia vijiji 12, Halmashauri ya Lindi imetekeleza/inatekeleza miradi 7 inayohudumia vijiji 13 kati ya hiyo, miradi 6 imekamilika na mradi 1 unaendelea na ujenzi upo katika hatua za mwisho za majaribio.

Manispaa imetekeleza miradi 7 inayohudumia  mitaa 20 na yote imekamilika na kutoa huduma, Liwale imetekeleza jumla ya miradi 6 inayohudumia vijiji 9 ambayo yote imekamilika na kutoa huduma, Nachingwea imetekeleza miradi 7 inayohudumia  vijiji 7 na Halmashauri ya Ruangwa imetekeleza miradi 5 ambayo imekamilika na inahudumia vijiji 12. Jumla ya miradi 38 ujenzi wake umekamilika, mradi 1 ujenzi wake upo katika hatua za majaribio, Jumla ya vijiji 71 vinanufaika na huduma ya Maji.

1.1.3 Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya II (WSDP II)

Mkoa wa Lindi unatekeleza programu ndogo ya maji na usafi wa mazingira awamu ya II ambapo hadi kufikia Agosti, 2018 hali ya utekelezaji ni kama ifuatavyo:-

  1. Kilwa DC: Miradi 7 inayohudumia vijiji 12 ujenzi umekamilika na Wananchi wanapata huduma. Utafiti wa maji chini ya ardhi umefanyika katika vijiji 17 na maeneo ya kuchimba visima  yamebainishwa kwa ajili ya maandalizi ya miradi ya 2018/2019.
  2. Lindi DC: Miradi 6 inayodumia vijiji 8 ujenzi wake umekamilika na huduma imeanza inatolewa. Miradi 1 unaohudumia vijiji 5 ujenzi wake unaendelea na upo hatua ya majaribio. Kijiji 1 kilikosa chanzo, juhudi za kutafuta chanzo zinaendelea kupitia awamu ya II ya Programu ya maendeleo ya Sekta ya maji. Usanifu umekamilika katika vijiji 4 vya Narwadi, Mkanga II, Lihimilo na Litingi. Aidha, Halmashauri imetangaza zabuni ya uchimbaji wa Visima na kufunga Pampu za Mkono katika vijiji 25. Kwa sasa mzabuni wa kazi hiyo ameshapatikana na kazi ya uchimbaji inatarajiwa kuanza Septemba, 2018.
  3. Lindi MC: Miradi 7 inayohudumia Mitaa 20 ujenzi wake umekamilika na huduma imeanza kutolewa. Kupitia awamu ya II ya programu ya maendeleo ya Sekta ya Maji, Usanifu wa Miradi kwa ajili ya mitaa 16 umekamilika, Mikataba ya miradi 2 itakayohudumia mitaa ya Mtutu, Nandambi, Narunyu, Tandangongoro na Muungano ipo hatua ya kusaini mikataba, mradi unatarajia kuanza mwezi septemba 2018.
  4. Liwale DC: Miradi 6 inayohudumia vijiji 9 ujenzi wake umekamilika na wananchi wanapata huduma. Miradi mipya 2 inaendelea na ujenzi, kipule(65%) na ndunyungu(60%)
  5. Nachingwea DC: Miradi 7 inayohudumia vijiji  7 ujenzi wake umekamilika, vijiji 3 vilikosa vyanzo vya maji lakini vimeingizwa katika awamu ya II ya Programu ya maendeleo ya Sekta ya maji, Miradi mipya 4 inaendelea na ujenzi, Chimbendenga(15%), Mtua(15%), Ndomoni (10%), Mandawa (5%) na inatarajiwa kukamilika mwezi Januari, 2019.
  6. Ruangwa DC : Miradi 5 inayohudumia vijiji 12 kati ya 13 imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji, kijiji 1 kilikosa chanzo (Chimbila B). Zoezi la kutafuta vyanzo vya maji limefanyika na Chanzo chenye maji ya kutosha kimepatikana. Miradi mipya 4 ambayo itatekelezwa kupitia awamu ya pili ya Programu ya maendeleo ya Sekta ya maji ipo katika hatua ya mapitio ya mikataba kabla ya kusainiwa na inatarajia kuanza kutekelezwa septemba 2018.

 1.2  Usajili wa Vyombo vya Watumiaji Maji

Katika kuhakikisha miradi ya maji inakuwa endelevu, miradi yote inaendeshwa na wananchi wenyewe kupitia Vyombo huru vya Watumiaji Maji/Vikundi vinavyoundwa kisheria (COWSOs). Hadi Juni 2018 julma ya vyombo vya watumiaji Maji 150 vimeanzishwa na kusajiliwa katika Mkoa. Kilwa (22), Lindi (47), Manispaa (2), Liwale (36), Nachingwea (21) na Ruangwa (22).

    1.3  Hali ya huduma ya maji mji wa Lindi  

    1.3.1 Mji wa Lindi

Idadi ya watu wanaopata huduma ya Maji safi ni watu wasiopungua 68,976 sawa na asilimia 75%  ya wakazi wote waishio eneo la Manispaa ya Lindi. Hali ya huduma imeimarika, hii ni kufuatia kuanza kutoa huduma kwa mradi mpya wa maji kutoka chanzo cha ng’apa.

Huduma ya maji hutolewa kupitia vyanzo vya maji vya Ng’apa, Mnazi mmoja, Mtange, Tulieni, Mmongo, Sinde na Mbanja, hata hivyo wakazi wengi hulazimika kufuata  maji umbali mrefu kupitia Virula(Vioski) kutokana na baadhi ya maeneo kutofikiwa na mtandao wa maji.

 1.3.2 Mpango wa Uboreshaji wa Huduma ya Maji katika Mji wa Lindi (Mradi wa Maji Ng’apa)

Serikali imepata ufadhili kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya kupitia Millenium Development Goal Initiative wa Euro Milioni 13.5 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji safi na usafi wa mazingira katika manispaa ya  Lindi. Gharama hizi ni pamoja na kazi za nyiongeza (Variations). Mradi huu unatekelezwa kwa kushirikiana na serikali ya Ujerumani kupitia KfW (Benki ya Maendeleo ya Ujerumani)

1.3.2.1 Kazi zilizopangwa kufanyika

Kazi zinazopangwa kufanyika ni: uchimbaji wa visima virefu 10; ujenzi wa chujio (aerator, contact basin/balancing tank, rapid sand filtration, clear water reservoir, high lift pumping station, backwash pumping station) lenye uwezo wa kusafisha maji mita za ujazo 7,500 kwa siku; ujenzi wa matanki mawili ya maji yenye ukubwa wa mita za ujazo 3,000 na 2000, ulazaji wa bomba kuu la maji umbali wa kilomita 11.5 na mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 27; ujenzi wa vituo vya kuchota maji na ujenzi wa mabwawa ya kutibu maji taka na ununuzi wa gari la huduma ya uondoaji majitaka.

 1.3.2.2 Hatua iliyofikiwa

  • Uchimbaji wa visima 8 vyenye urefu wa mita 80 - 120 vyenye uwezo wa kuzalisha mita za ujazo 7,500 kwa siku umekamilika na maji ya kutosha kukidhi mahitaji ya Manispaa ya Lindi  yamepatikana. Visima  vyote 8 vimefungwa pampu na kuunganishwa, kati ya hivyo kisima 1 kinafanyiwa marekebisho katika mfumo wa umeme (Contactor na Starter).
  • Matanki yote ya kuhifadhia maji yamekamilika (mita za ujazo 3000 na 2000) na mabomba ya kupeleka maji katika matanki na kusambaza maji yamekamilika pamoja na  maunganisho.
  • Ujenzi wa chujio (aerator, contact basin/balancing tank, rapid sand filtration, clear water reservoir, high lift pumping station, backwash pumping station na majengo ya utawala umefanyika.
  • Ujenzi wa vituo vya kuchotea maji vya umma 13 ambapo 10 kati ya hivyo vinatoa huduma eneo la kilimahewa.
  • Mabwawa ya kutibu maji taka yamejengwa eneo la mitwero na gari la majitaka limeagizwa.
  • Hadi mwezi agosti 2018, mradi umefikia asilimia 90 ya utekelezaji.

1.3.2.3 Kazi zinazoendelea

Kuunganisha mfumo wa automation katika mfumo wa kutibu maji (Water treatment plant)

Kuunganisha mabomba ya usambazaji katika mitaa ya muhimbili, Nachingwea na Rahaleo.

Maeneo ambayo yameanza kupata huduma kutoka mradi wa Maji Ng’apa

Baadhi ya maeneo yanayonufaika ni Mjini kati, Mtanda, Wailes, Mtuleni, Mpilipili kusini, Angola, Majanimapana, Usalama, gerezani, sabasaba, Rada, baadhi ya maeneo ya Mlandege, Nachingwea na Kilimahewa (ambapo kuna vituo vya kuchotea maji).

    1.5.3 Mradi wa Maji Ng’apa Mtaa wa Ng’apa na Mtaa wa Mitwero

Katika kuhakikisha huduma ya maji inaboreshwa katika Manispaa ya Lindi, Serikali katika bajeti yake ya 2018/19 imeitengea LUWASA kiasi cha shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi miwili ya maji.

  • Mradi wa maji wa Ng’apa Mtaa wa Ng’apa na
  • Mradi wa kufikisha huduma ya maji eneo la Mitwero.

Kwa mradi wa Mtaa wa Ng’apa ambao mchakato wake wa manunuzi unasimamiwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji, zoezi la kumpata mkandarasi wa ujenzi lipo katika hatua za mwisho kukamilika.

Lakini pia kwa upande wa mradi wa Mitwero Mamlaka tayari ilishawaisilisha andiko la mradi (Project proposal) Wizarani na kinachosubiriwa ni kupata kibali cha kuendelea na taratibu za manunuzi ili taratibu za kumpata mkandarasi zianze.

Hitimisho

Mradi huu utakapokamilika utazalisha  maji mita za ujazo 7500 kwa siku (Lita 7, 500,000 kwa siku) na utaongeza huduma ya maji safi na usafi wa mazingira katika mji wa Lindi.

 Hali ya huduma za Maji katika Miji Mikuu ya wilaya

Wastani wa upatikanaji wa huduma ya maji kwa maeneo ya mjini ni 67.96% na upotevu wa maji ni 32.2 %. Takwimu za kila wilaya zinaonyesha kuwa upatikanaji wa huduma Kilwa Masoko ni 80% na kiwango cha upotevu ni 33%. Manispaa ya Lindi upatikanaji ni 75% na upotevu ni 32%, Liwale upatikanaji ni 58% na upotevu ni 32%, Nachingwea upatikanaji ni 71.4% na upotevu ni 29%, Ruangwa  upatikanaji ni 55.4 % na upotevu ni 35%. Upotevu wa maji kwa kiasi kikubwa unasababishwa na uchakavu wa miundombinu ya maji, wateja kutofungiwa dira za maji na mivujo ya mara kwa mara.

Mikakati ya kupunguza upotevu wa maji 

  • Kuwa na kikundi maalumu kilichowezeshwa kudhibiti mivujo kwa wakati na haraka (usafiri na vifaa).
  • Kubadili miundombinu iliyochakaa (bomba na viungio).
  • Kufunga mita kwenye vituo vya uzalishaji na usambazaji maji.
  • Kuwafungia mita wateja wote.
  • Kutambua wateja wanaotumia maji kinyume na kuwahalalisha.
  • CHANGAMOTO ZA SEKTA YA MAJI 

Mkoa wa Lindi unakabiliana na changamoto zifuatazo katika utoaji wa huduma za maji;-

1.6.1  Changamoto za  Utekelezaji wa  Miradi ya  Maji Vijijini

Upatikanaji wa shida wa vyanzo vya maji. Sehemu kubwa hupatikana maji yasiyofaa kwa matumizi ya binadamu au mbali na maeneo ya wakazi hivyo kufanya gharama za ujenzi wa miradi ya Maji kuwa kubwa.

Dhana ya maji kuwa huduma ya bure bado imo miongoni mwa watumiaji maji wa vijijini na hivyo kukwamisha uanzishaji wa vyombo huru vya watumiaji maji.

Upungufu wa watumishi wa maji katika halmashauri na mkoa. Halmashauri zilizo athirika zaidi ni Kilwa, Ruangwa, Lindi DC na Lindi MC

Upatikanaji usiokuwa wa uhakika wa vipuri na vifaa vingine vya miradi ya maji vijijini.

  • Uharibifu unaofanywa katika vyanzo vya maji.
  • Mabadiliko ya tabia nchi hali inayopelekea baadhi vyanzo vya maji kukauka hasa visima.

 1.6.2  Mipango/Mikakati ya kukabiliana na changamoto 

Elimu juu ya Sera ya Maji ya Taifa ya mwaka 2002  inaendelea kutolewa kwa watumiaji maji vijijini na kuwashirikisha kikamilifu wananchi wanufaika katika hatua za kubuni na kujenga miradi yao ya maji.

Kuhusu upungufu wa watumishi, serikali imeanza kuajiri wahandisi na mafundi mchundo na kuwapeleka katika Mkoa na Halmashauri zetu.

Kuhusu upatikanaji wa vipuri vya mitambo ya maji, Halmashauri zimeshauriwa kuwashirikisha wafanyabiashara waliopo katika maeneo yao ili kuwa tayari kuweka katika maduka yao vipuri vya mitambo ya maji, mabomba ya maji pamoja na viungio vyake.

Halmashauri zinaendelea kuwahimiza wananchi kuvuna maji ya Mvua na zimeanza kutunga sheria ndogo za uvunaji maji ya mvua ili kupunguza tatizo la uhaba wa maji.

Kuhusu utunzaji wa vyanzo vya maji elimu inaendelea kutolewa juu ya umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji na kuwaondoa wale wote wanaolima karibu na vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kuwachukila hatua za kisheria wanaochoma moto maeneo yenye vyanzo vya maji ikiwemo ufyatuaji wa matofali. 

 

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.