Wajasiriamali wadogo kutoka katika Halmashauri za Lindi Manispaa na Mtama wanufaika kwa kupatiwa mafunzo ya manunuzi ya umma kwa njia ya kielectroniki, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuhakikisha makundi maalumu yanashiriki kikamilifu katika tenda za serikali ambazo zinatengwa kwa asilimia 30 kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo,Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Ndugu. Juhudi Mgallah amewapongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa kuwafungulia njia na kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo ili waweze kukuza mitaji yao na vipato vyao kupitia zabuni zinazotolewa na serikali.
"Tunaamini kwamba mafunzo haya yanakwenda kuwapa chachu ya kuboresha huduma zenu ili kuweza kuweka ushindani katika tenda zinazotangazwa na serikali kwa ajiri ya makundi maalumu kwa mujibu wa sheria. Vilevile, tunawaomba mukawe walimu na mabalozi kwa wajasiriamali wenzenu ambao bado hawajapata mafunzo haya, lengo ni wajasiriamali wote waweze kupata nafasi ya kushiriki na kutoa huduma kwa serikali" Ndg. Mgallah.
Aidha, Mgallah amewataka wajasiriamali hao kuwa mstari wa mbele kudumisha na kuenzi amani ya nchi hususan katika kipindi hiki cha uchaguzi na kutoa taarifa za viashiria vya uchochezi na uvunjifu wa amani kwa serikali na kuacha kufata mikumbo.
“Tunapokwenda kupiga kura tarehe 25 Oktoba, tuhakikishe tunashiriki uchaguzi kwa amani, tuache kuwa vichochezi wa uvunjifu wa amani na uanzishaji wa vurugu, tuache kufuata mikumbo kwa usalama wetu na familia zetu,tuhakikishe tunatii sheria na kuwasikiliza viongozi” aliongeza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.