Shilingi bilioni 7.8 zinatarajiwa kutumika kujenga na kukarabati miradi mbalimbali ya sekta ya elimu katika Halmashauri ya Mtama, mkoani Lindi. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 4.1 zinatoka serikali kuu, bilioni 3 kutoka kwenye Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP), na milioni 719 kutoka kwenye Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Shule za Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST).
Miradi inayotarajiwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa shule ya wavulana kanda ya Kiwalala, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya choo katika Shule ya Msingi Mahumbika, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya choo katika Shule ya Msingi Chiuta, na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya choo katika Shule ya Msingi Mandwanga. Pia kutakuwa na ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Mtakuja, ukarabati wa madarasa matano katika Shule ya Msingi Simana, ujenzi wa Shule ya Sekondari Navanga, na ujenzi wa Shule ya Amali Mpenda.
Miradi mingine ni ujenzi wa madarasa matano katika Shule ya Msingi Simana, ujenzi wa Shule ya Sekondari Mtakuja katika Kata ya Nyangao, ujenzi wa shule mpya ya amali mkoa, na ujenzi wa Shule ya Sekondari katika Kata ya Pangani.
Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua uendelevu wa miradi hiyo na kuona maandalizi ya kuripoti kwa wanafunzi wa darasa la kwanza, awali, na kidato cha kwanza, Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Zuwena Omary, ametoa wito kwa menejimenti ya halmashauri kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.
Aidha, amesisitiza kuhakikisha wanafunzi wote waliopangiwa na kuandikishwa wanaripoti shuleni kwa wakati..
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtama Anderson Msumba amesema wanamshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi alizowaletea , kwa mara ya kwanza kupata fedha nyingi kama hizo na amwakikishia Katibu Tawala Mkoa kukamilisha miradi hiyo mwishoni mwa mwezi wa Nne.
Mwakilishi wa wenyeviti kutoka Halmashauri ya Mtama Juma Omari Salumu wa kijiji cha Kiwalala amemshukuru Mhe. Rais kwa mradi huo na kuahidi kutoa ushirikiano kwa wananchi na viongozi wote.
Brigita John Mponda mkazi wa kijiji hicho kwaniaba ya wananchi amesema miradi hiyo wameipokea vizuri miradi ujenzi wa shule mpya kwani inakwenda kuwaletea elimu bora kwa watoto wao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.