• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

DC NGOMA ASHIRIKI ZOEZI LA UPANDIKISHAJI VIFARANGA VYA SAMAKI 7000 KATIKA MABWAWA YA UFUGAJI KIJIJI CHA NAHANGA- RUANGWA

Posted on: October 29th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hassan Ngoma, leo Octoba 29, 2024 akimuwakilisha Mhe. Zainab Telack, Mkuu wa Mkoa wa Lindi amezindua rasmi zoezi la upandikizaji wa vifaranga vya samaki katika mabwawa mawili ya kufugia samaki yaliyopo Kijiji cha Nahanga, Kata ya Mandawa, Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ambapo jumla ya vifaranga 7,000 vimepandikizwa.


Akisoma risala ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Ngoma amepongeza juhudi za Serikali katika kuanzisha mradi wenye thamani ya Tsh. Milioni 128 ambao unaratibiwa na  Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu chini ya Programu chini ya Programu ya Lishe na Ufugaji endelevu ambapo ameeleza kuwa mradi huo ukitumiwa vyema kwa malengo yaliyokusudiwa utakwenda kubadilisha maisha ya wakazi wa kata ya Mandawa kwa kuongeza kipato, kutoa fursa za ajira na kuboresha lishe miongoni mwa wanajamii na kuongeza kuwa mradi huo utakuwa kichocheo muhimu cha maendeleo katika sekta ya uvuvi wilayani Ruangwa.


Aidha, Mhe. Ngoma ametoa wito kwa wanakikundi wanufaika wa mradi huo na wanajamii kwa ujumla kuhakikisha mradi huo unakua endelevu na unakua wenye manufaa kama yalivyo malengo ya serikali ambayo imeendelea kujipambanua kwa kubuni miradi mbalimbali ya kiuchumi ili  kuhakikisha inaboresha maisha ya wananchi wake hususan kuongeza wigo wa fursa za kujiajiri kwa vijana na wanawake.


Ili kuhakikisha mradi huo unakua endelevu, Mratibu wa Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi Tanzania,amewasisitiza wanakikundi kuhakikisha wanazingatia elimu ya ufugaji wa samaki waliyoipata kupitia mafunzo hususan utengenezaji wa chakula cha samaki na namna ya kuwalisha pamoja na ulinzi wa mabwawa dhidi ya wanyama waharibifu kama Kenge na ndege walao samaki.


Akimuwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Bwana. Nathalis Linuma amewataka wananchi kuutunza mradi na kuhakikisha moja ya faida yake kubwa ni kuimarisha lishe za wakazi wa kata ya mandawa pamoja na kujiongezea kipato, na kuwasisitiza kushiriki katika zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu.


Mzee Mwigambe, Mkazi wa Kijiji cha Nahanga ameishukuru serikali kwa kuwaletea mradi huo wenye manufaa kiuchumi na kijamii na kuwaomba wananchi wenzake kushirikiana na kuunga mkono juhudi za serikali bila ya kubagua itikadi za vyama vya siasa bali kuangalia mwenendo wa maendeleo yanayopatikana katika maeneo yao. 

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.