Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainabu Telacky, leo tarehe 04/03/2025 amefanya ziara Wilayani Kilwa kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bandari ya uvuvi inayojengwa katika eneo la Kilwa Masoko.
Katika ziara hiyo, Mhe. Telacky amepongeza hatua nzuri iliyofikiwa katika ujenzi wa mradi huo muhimu kwa maendeleo ya sekta ya uvuvi na uchumi wa wakazi wa Kilwa na mkoa wa Lindi kwa ujumla. Amesisitiza kuwa kukamilika kwa mradi huu kutatoa fursa kubwa kwa wavuvi na kuchochea ukuaji wa biashara ya uvuvi.
Aidha, Mheshimiwa Telacky amezitaka mamlaka husika ndani ya Wilaya ya Kilwa kuhakikisha kuwa miundombinu ya huduma za msingi zinapatikana katika eneo la mradi, ambapo amewataka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kuhakikisha maji safi yanapatikana katika eneo hilo kwa wakati, ili kuwezesha utekelezaji mzuri wa shughuli zitakazofanyika bandarini hapo.
Vilevile, Mkuu wa Mkoa amewataka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha wanafikisha huduma ya umeme katika eneo hilo kwa haraka ili kuwezesha shughuli za ujenzi na uendeshaji wa bandari hiyo kwa ufanisi.
Ziara hii ni sehemu ya jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, za kuhakikisha miradi ya kimkakati inatekelezwa kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
@ortamisemi
@ikulu_mawasiliano
@maelezonews
@
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.