Jamii Mkoani Lindi imehamasishwa kujiwekea utaratibu wa kuhakikisha wanapanda miti katika maeneo yao ili kurejesha uoto wa asili,kujipatia lishe na kupunguza madhara ya mmomonyoko wa ardhi katika maeneo mbalimbali.
Uhamasishaji huo umefanywa jana Machi 20,2024 wakati wa uzinduzi kampeni ya Kimkoa ya upandaji miti ambayo imezinduliwa katika eneo la jengo jipya la halmashauri ya Mtama lililopo Mtaa wa Majengo B Kijiji cha Mtama.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Majid Myao amesema mazingira na rasilimali misitu vimeharibiwa kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu kama kufyeka misitu na kuchoma moto mashamba vitendo ambavyo vimesababisha madhara yakiwemo mabadiliko makubwa ya hali ya hewa ambayo yalisababisha vyanzo vya maji kukauka,mvua kubwa na ongezeko kubwa la joto duniani.
Kwa upande wake Afisa Misitu Zawadi Jilala amesema Mkoa wa Lindi umepangiwa lengo la kupanda miti 9,000,000 kila mwaka ,lakini kila Wilaya inalengo la kupanda miti 1,500,000.
Amesema kwa mwaka 2022/2023 Manispa ya Lindi wakiwa wenyeji uzinduzi wa kampeni hiyo jumla ya miti 5,555,155 ambayo ni sawa na asilimia 62 ya utekelezaji wa lengo na katika hiyo miti 4,834,483 ilipona sawa na asilimia 87 ya miti iliyopandwa huku kwa mwaka huu 2023/2024 ikiwa zamu ya Wilaya ya Lindi kwa halmashauri ya Mtama kuwa wenyeji wa uhamasishaji wa upandaji wa miti kupitia kampeni hiyo ya Kimkoa zaidi ya miche 400 imepandwa kuzunguka eneo la jengo la ofisi mpya ya halmashauri hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.