Wito umetolewa na katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi Zuwena Omary wa kufanya mazoezi ya viungo na kushiriki usafi wa mazingira ."Nitawaomba Jumamosi ya wiki ijayo, kwanamna ambavyo tutakuwa tumejipanga tukishafanya mazoezi yetu twende sehemu fulani tukafanye usafi kidogo, baada ya hapo tutakutana nyumbani kwako, mtaani kwako au ofisini kwako kuulizana umesaidiaje kufanya eneo lako kuwa safi " Katibu Tawala Bi Zuwena OmaryKatibu tawala ametoa wito huo leo Julai 13, katika viwanja vya mazoezi Ilulu mara baada ya mazoezi ya viungo ambayo yanafanyika kila siku ya J'mosi kuanzia saa 12:00 asubuhi uwanja wa Ilulu.Utaratibu huo wa mazoezi ni endelevu ukihusisha wananchi , Taasisi mbalimbali na vikundi vya mazoezi (Jogging Club ) .Aidha, amewapongeza wote ambao wameshiriki mazoezi hayo na kumpongeza afisa michezo ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa usimamizi wa utaratibu huo na kusisitiza kuwa endelevu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.