• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

KATIBU TAWALA LINDI AWATAKA WANAJAMII KUSHIRIKIANA KUDHIBITI MATUKIO YA UNYANYASAJI WA WATOTO.

Posted on: December 8th, 2022

Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Ndg. Ngusa D. Samike amewataka wazazi, walezi na wanajamii  kushirikiana katika kudhibiti matukio mbalimbali ya unyanyasaji kwa watoto ikiwemo ubakaji na ulawiti kwa watoto wa kiume ambayo hufanywa na watu wanaoaminika miongoni mwa wanajamii hao.

Katibu Tawala ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa- Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) kwa muda wa robo ya kwanza iliyoanza mwezi Julai hadi Septemba 2022, kilichofanyika katika ukumbi wa mkutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi.

“Matishio ya malezi na makuzi ya mtoto yamezidi kuongezeka katika jamii zetu, na katika kipindi hiki cha watoto wengi hasa wa kiume ndio waliopo katika hatari zaidi za kufanyiwa vitendo hivi vya ukatili hususani matukio ya ulawiti, na watu wanaofanya matukio haya ni wale ambao jamii imekuwa ikiwaamini na kuwapa jukumu la kuwalea na kuwatunza watoto hawa ikiwemo ndugu wa karibu na muda mwingine viongozi wa dini ambao ndio tunawaamini sana”

Awali, akitoa taarifa ya robo mwaka ya Mkoa ya utekelezaji wa PJT-MMMAM, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Bwana. Gaudence Nyamwihura amesema mpango unajumuisha maeneo sita ambayo ni Afya, Elimu, Lishe, Ulinzi na Usalama, Malezi yenye Mwitikio na Uhamasishaji wa Programu ya PJT-MMMAM na  unatekelezwa kwa kupitia ngazi za Halmashauri 6 za mkoa wa Lindi.

“Katika utekelezaji za afua za lishe, program imeongeza uhamasishaji wa wazazi na walezi kuchangia chakula mashuleni kwa madarasa ya awali na vituo vya kulelea watoto mchana katika kata nne za Halmashauri ya Liwale, ambapo katika kipindi cha Julai-Septemba 2022 jumla ya Tsh, 3,460,000 zilikusanywa na wananchi na kugharamia chakula cha mchana kwa watoto wa madarasa ya awali.”

Aidha, Bwana Nyamwihura ametoa pongezi kwa Halmashauri ya Kilwa kwa hatua za utekelezaji wa program hii ambapo tayari wameshaanza kutenga vifungu vya fedha kwa ajiri ya kuchangia chakula mashuleni na Halmashauri ya Manispaa ya lindi kwa kutoa elimu ya bustani ya mbogamboga na matunda kwa wanufaika wa TASAF ili kuhakikisha familia na  watoto wao wanapata mlo kamili.

  

 


Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.