Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Zuwena Omari akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amepongeza Maandilizi mazuri ya mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru Kwa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
Pongezi hizo zimetolewa Mei 17, 2025 mara baada ya kutembelea na kukagua miradi ya Mwenge Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa lodge ya sofishaka iliyopo kata ya Mingoyo, Ujenzi wa shule ya Sekondari Hamida El qassim iliyopo kata ya Rasbura yenye vyumba viwili vya maabara ya kemia na baiolojia,maabara ya fizikia ,jengo la Utawala,madarasa manane, matundu ya vyoo,Jengo la la ICT na Library, pamoja na, Ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi.
Miradi mingine ni Kikundi Cha Vijana cha mapambo (Salumu Decoration) kilichopo kata ya Matopeni ,Ujenzi wa Bara bara Kwa kiwango cha lami kuelekea shule ya Sekondari Lindi Wasichana iliyopo kata ya Kilangala pamoja na Ujenzi wa jengo la NHIF, lililopoa kata ya Rasbura.
Katika hatua nyingine katibu tawala Mkoa wa Lindi ame upongeza Umoja wa Vijana Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Kwa hamasa kubwa na Maandilizi mazuri kuelekea mapokezi ya mbio za mwenge wa Uhuru siku ya tarehe 27 Mei, 2025 na kuwaomba waendelee na hamasa hiyo mpaka siku ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.
“Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 Kwa Amani na Utulivu “
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.