Mwenyekiti wa kamati ndogo za Maandalizi ya Maonesho ya Nanenane kanda ya kusini Ndugu Mwinjuma Mkungu ambaye katibu Tawala Msaidizi Uchumi na uzalishaji ameongoza kikao cha kamati ya maandalizi ya maonesho ya Nanenane ambayo yanatarajiwa kufanyika uwanja wa Nanenane Kanda ya Kusini Ngongo Agosti 8, 2025.
Kikao hicho ni miongoni mwa maandalizi ya kikao kikubwa kitakachokutanisha wajumbe kutoka mikoa yote shiriki ambacho kinatarajiwa kufanyika tarehe 9 Julai ,2025 katika viwanja vya Nanenane Ngongo .
Maonesho ya Nanenane mwaka huu yamebeba kauli mbiu inayosema " Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo , Mifugo na Uvuvi 2025 "
Aidha, Mwenyekiti amewataka wajumbe kuendelea kujipanga kuhakikisha maonesho ya msimu huu 2025 yanafana .
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi mdogo ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.