KIKAO CHA MAANDALIZI YA HAFLA YA UTOAJI VYETI NA VIFAA KWA WAHITIMU WA KOZI YA WATOA HUDUMA ZA AFYA NGAZI YA JAMII- WAJA
Posted on: September 7th, 2025
Mganga Mkuu Mkoa wa Lindi Dkt. Kheri Kagya ameongoza Kikao cha Kujadili Maandalizi kuelekea hafla ya utoaji wa Vyeti kwa Wahitimu wa Mafunzo kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii itakayofanyika tarehe 8, Septemba, 2025 Mkoani Lindi.
Wataalamu kutoka Wizara ya Afya wakiongozwa na Bahati Mwailafu ,Timu ya Uendeshaji Huduma za Afya Ngazi ya Mkoa (RHMT's) wameshiriki
Kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi iliyopo Hospitali ya Sokoine Manispaa ya Lindi .
Vyeti vitatolewa kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii baada ya kusoma vyuo vya afya kwa ufadhili wa Serikali kwa kipindi cha miezi 6 kupitia Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii uliozinduliwa na Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango tarehe 31, Januari, 2024.