Leo Julai 11, Mkoa wa Lindi umefanya kikao cha tathmin ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Elimu kwa mwaka 2025 kwa kipindi cha nusu muhura yaani kuanzia Januari hadi Juni 2025 ikiwa ni sehemu ya kuangazia mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto na kuzitafutia ufumbuzi ili kuweza kufikia malengo ya Mpango huo.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Katibu Tawala Msaidizi Elimu, Mwl. Joseph Mabeyo ameeleza kuwa kikao hiko ni muhimu kwakua kinasaidia kupata taswira ya utekelezaji wa malengo kwa kuakisi mikakati iliyopangwa, utekelezaji wake, mafanikio, changamoto na nini kifanyike ili kutatua changamoto hizo.
"Ni utamaduni wetu kufanya tathmini ya mpango mkakatu wa elimu katika ngazi zote kuanzia Kata, Wilaya, Halmashauri hadi Mkoa ili tuweze kupata taswira ya pamoja ya nini kimefanyika kulingana na tuliyoyapanga, tulichofanikiwa na wapi tulikwama ili tupeane uzoefu wa namna ya kukabiliana na changamoto hizo ili kwa pamoja tuweze kufikia malengo tuliyojiwekeza" ameeleza.
Katika kikao hicho kilichowakutanisha viongozi wa elimu wa ngazi mbalimbali wakiwemo Maafisa Elimu Msingi na Sekondari, Maafisa Elimu Kata, Maafisa Michezo na Utamaduni, Wadhibiti ubora wa shule pamoja na Walimu Wakuu wa Shule, kinatarajiwa kutoka na Maadhimio yatakayosaidia utekelezaji na kuleta matokeo yanayotarajiwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.