• Wanawake wahamasishwa kuunga mkono ajenda ya serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati safi kupikia.
Wanawake wa Mkoa wa Lindi wameungana na wanawake wote nchini na duniani kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani 2025 ambapo katika Mkoa wa Lindi maadhimisho hayo yamefanyika kimkoa wilayani Nachingwea na kujumuisha wanawake kutoka taasisi mbalimbali za serikali, sekta binafsi, wajasiriamali na wananchi.
Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Mohamed Moyo, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea ametumia maadhimisho hayo kuwakumbusha wanawake jukumu lao la msingi la matunzo na malezi kwa watoto kwa kuzingatia mila na tamaduni za kitanzania na kuhakikisha wanapeleka watoto shule ili wapate elimu bora.
Aidha, Mhe. Moyo ameeleza kuwa serikali ya awamu ya sita inaendelea kuwawezesha wanawake kwa kuwasogezea fursa mbalimbali za kiuchumi ili waweze kukuza vipato vyao binafsi ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo isiyo na riba ya halmashauri pamoja na kushirikiana na madirisha mbalimbali ya taasisi za kifedha za kibenki inayotoa mikopo ya riba nafuu na elimu za ujasiriamali ili mwanamke yoyote asikwame kujikwamua kiuchumi kwa kukosa mitaji.
Wanawake pia wamehamasishwa ushiriki wao katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, kwa kujitokeza kuwania nafasi za udiwani na ubunge ili wapate nafasi ya kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Kwa mwaka 2025 inasema "Wanawake na wasichana 2025,tuimarishe haki usawa na Uwezeshaji"
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.