Akiwasilisha taarifa ya uendeshaji wa zao la korosho kwa Mwaka 2024/2025, Katibu Tawala Msaidizi, uchumi na uzalishaji Mkoa wa Lindi Ndugu, Mwinjuma Mkungu ameeleza kuwa, Mkoa wa Lindi umeuza tani 115,680 za korosho ghafi zenye thamani ya Shilingi Bilioni 364.38 katika msimu wa 2024/2025.
Ndugu Mkungu ameyaeleza hayo hayo Agosti 22/2025 katika Mkutano Mkuu wa wadau wa Tasnia ya korosho unaofanyika Jijini Dodoma.
Katika kuhakikisha Mkoa wa Lindi unaongeza uzalishaji wa zao la korosho, Mkoa umeweka mikakati kabambe ikiwemo kuondoa mikorosho ya zamani ambayo imezeeka na kuzalisha miche bora ya zao hilo ili kuongeza uzalishaji, alieleza Ndugu Mkungu.
■ _Huku Mtama ikiibuka na ushindi wa kuwa halmashauri inayofanya vizuri katika kusimamia mikakati ya wakulima wa korosho, kuendeleza na kusaidia wakulima wa zao hilo kufikia lengo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.