Kutokana na ongezeko la uharibifu wa Mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na athari za kiafya zinazotokana na matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia , Matumizi ya nishati safi ya kupikia ni ajenda mahususi ambayo imechukua nafasi kubwa katika sera, Mipango na Mikakati ya Serikali mbalinbali duniani.Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ajenda ya kitaifa ya Matumizi ya Nishati safi ya kupikia ikisimamiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alielekeza kuandaliwa kwa mkakati wa Taifa utakaotoa mwongozo wa Matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo ifikapo 2034 watanzania zaidi ya 80% watumie nishati hiyo .
Wakala wa nishati safi ya kupikia (REA) unatekeleza mkakati huo kwa vitendo, ambapo leo agosti 3, 2025 Kaimu Meneja Msaidizi wa ufundi kwa waendelezaji wa Miradi Mhandisi. Emmanuel Yesaya ametambulisha mtoa huduma wa uuzaji wa majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku mbele ya katibu Tawala Mkoa wa Lindi ambapo jumla ya majiko 16,275 yatauzwa kwa bei ya Tsh elfu 19,500, yenye thamani ya Mil 317.3.
Mhandisi Emmanuel amesema kuwa, wakala wa Nishati Vijijini (REA umeingia mkataba na Mtoa huduma kampuni ya Taifa Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi huo, ambapo halmashari zote zitafikiwa na mtoa huduma ikiwa lengo kufikia mpango na mkakati wa Taifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kabla ya 2034 ili kunusuru afya za wananchi na mazingira.Kwa upande wake katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena omary ameendelea kumshukuru Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusimamia mpango huo kwa watanzania wakiwemo wa Mkoa wa Lindi kwasababu majiko hayo ya gesi yanakwenda kuwa msaada mkubwa kwa kurahisha upikaji na kupunguza muda mwingi wa kutafuta kuni ama mkaa ambao unaathari kwa afya na mazingira .
Aidha , ametoa wito kwa wananchi kujaza mitungi ya gesi pale inapoisha ili kuendelea kutumia nishati safi.Ametumia fursa hiyo kutoa maelekezo kwa mtoa huduma Taifa Gas kusambaza mawakala wa huduma hiyo kila kata ili kuwarahishia wananchi kupata huduma hiyo.
Naye Meneja Mauzo Kanda ya Kusini Bi Hawa Omary Juma ameeleza namna walivyojipanga katika kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kirahisi.@wakalawanisha
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.