Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Lindi, Ndg. Charles Kigahe, ameeleza kuwa lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo kushiriki na kupata tenda za serikali kupitia mfumo wa Nest.
“Mafunzo haya yanatarajiwa kuwapa uelewa wa namna ya kuingia kwenye mfumo wa NeST na kushiriki tenda bila kushindana na wafanyabiashara wakubwa. Tunatarajia mtaenda kuwa mawakala wazuri wa maendeleo kwa kutumia maarifa haya kwa manufaa yenu na jamii kwa ujumla,” alisema Kigahe.
Mafunzo haya pia yameambatana na maelekezo ya mfumo wa NeST yanayokusudia kukutanisha makundi maalumu ya watoa huduma za zabuni na taasisi za ununuzi ili kurahisisha mchakato wa kutangaza na kushiriki zabuni.
Ni matarajio ya Serikali kwamba baada ya mafunzo haya, wajasiriamali wadogo wataweza kuomba na kushinda tenda za serikali kwa wingi zaidi, hatua ambayo itakuza biashara zao na kuongeza uchumi wa Mkoa wa Lindi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.