Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena omary ameungana na viongozi mbalimbali wa Serikali ngazi ya Kanda, viongozi wa dini, Mkoa , wilaya, Taasisi, Mashirika pamoja wananchi kuaga mwili wa aliyekuwa Meneja wa TANESCO Mkoa wa Lindi Mhandisi Athumani Abdul Jumbe kwa ajili ya kuanza safari ya kusafirisha kuelekea Kisarawe Pwani ambako mazishi yatafanyika.Katibu Tawala Mkoa , akiwasilisha Salamu za Pole , kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa, amesema Mhandisi Athumani Abdul Jumbe atakumbukwa kwa mengi mazuri na tunapaswa kujifunza kutoka kwake namna alivyokuwa anafanya kazi zake katika utumishi wa umma. "Ofisi ya Mkuu wa Mkoa haijawahi kupokea malalamiko kutokana na utumishi au utendaji kazi wake , labda meneja wa TANESCO kafanya ili au lile , kwahiyo ninaomba watumishi wenzangu na wananchi wa Mkoa wa lindi tujifunze kupitia maisha ya wema aliyoishi Ndugu yetu Athumani Jumbe , na ndiyo maana kwa muda mfupi tumekutana hapa kutokana na wema aliotutendea ." Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Zuwena Omari.Ametumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi wa umma kutimiza majukumu waliyopewa ya kuwatumikia wananchi kwani maisha yetu hapa duniani ya muda tu .Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe. Victoria mwanziva akiwasilisha salamu za pole kwaniaba ya wakuu wa wilaya wote wa Mkoa wa Lindi, amesema walipohitaji ushirikiano kutoka kwa Meneja Jumbe wakati wowote ambapo taarifa au jambo la kiutendaji linapohitajika ama utatuzi wa changamoto katika kuwahudumia wananchi, walipata ushirikiano kwa wakati .Aidha, viongozi wa chama cha Mapinduzi , Tasisi, Meya wa Manispaa ya Lindi kwaniaba ya wenyeviti wote wa Halmashauri, Viongozi wa dini na Mashirika walipata wasaha wakuwasilisha salamu za pole na rambirambi .Apumzike kwa amani .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.