• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Mhe. Majaliwa akagua ukarabati shule ya msingi Mnacho

Posted on: May 9th, 2017

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amekagua ukarabati wa majengo unaoendelea kufanyika katika shule ya msingi Mnacho iliyopo Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.

Shule hii ilianzishwa mwaka 1965 na kabla ya ukarabati kufanyika majengo yake yalikuwa yamechakaa sana. Mhe. Majaliwa akiwa ni mmoja ya wanafunzi ambao wamesoma hapo mwaka 1970 kuanzia darassa la kwanza hadi la saba aliamua kutafuta wafadhili ambao ndio wamesaidia kufanya ukarabati na sasa majengo ya shule yamebadilika.

Baada ya ukaguzi, Mhe. Majaliwa aliongea na viongozi, walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Mnacho ambapo alianza kwa kuwapongeza walimu kwa uvumilivu waliouonyesha kwa kufanya kazi katika mazingira ya majengo chakavu. Pia aliwapongeza kwa kazi nzuri ya ufundishaji wanayoendelea kuifanya.

Aidha, aliwaeleza kuwa pindi ukarabati huu utakapokamilika shule kwa upande wa majengo itakuwa imeimarika na kuwa na mwonekano mzuri. “Najua bado zipo changamoto kwenye upande wa nyumba za walimu ambazo nazo zinahitaji ukarabati, ila niahidi kwamba ukarabati huu ukishakamilika eneo litakalofuata ni ukarabati wa nyumba za walimu kuanzia nyumba namba moja hadi namba tano” alisema Mhe. Majaliwa.

Vilevile aliwasihi wanafunzi kusoma kwa bidi ili na wao wakiwa wakubwa waweze kuja kushika nyadhifa mbalimbali kama yeye au hata zaidi. Pia aliwataka wanafunzi kuwaheshimu walimu wao na kuwa na nidhamu ya hali ya juu.

Kwa upande wa wananchi na viongozi waliokuwepo, Mhe. Majaliwa aliwaeleza kuwa ukarabati huu ni mwanzo wa ndoto aliyonayo ya kuboresha miundombinu ya shule hiyo. Aidha, amewasihi sana viongozi, wananchi na walimu kuwa na ushirikiano ili waweze kufanikiwa kuboresha elimu katika Wilaya nzima ya Ruangwa.

Pia Mhe. Majaliwa amewaomba waendelee kumuombea ili aweze kutimiza ndoto zake alizonazo za kuwa na Ruangwa yenye maendeleo na kuwa hilo litawezekana kama wanaruangwa wote wataungana na kuwa kitu kimoja.

Ukaguzi huu wa shule aliufanya baada ya kumaliza kushiriki mazishi ya aliyekuwa diwani wa kata ya Mnacho, Ndg Daniel Petro Mtawa ambae alifariki kutokana na ugonjwa wa moyo uliopelekea mwili kupooza upande mmoja.

Ambapo akiwa msibani aliwaomba watu kuendelea kumuombea marehemu, huku akiwasihi watu wote kujiandaa kama maneno ya mtumishi aliyoyasema ya watu kutenda matendo yaliyo mema yanayompendeza Mungu wakati wapo hapa duniani. “Nawapa pole sana wanafamilia, ndugu, jamaa, marafiki na madiwani kwa msiba huu uliotufika, msiba huu umetugusa sote kwani marehemu ni mtu ambaye tulikuwa tukishirikiana nae katika mambo mengi ya kimaendeleo katika wilaya yetu” alisema Mhe. Majaliwa.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.