• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

MHE. ULEGA AMEVITAKA VYAMA VYA USHIRIKA KUWA MKOMBOZI WA WAKULIMA, MIFUGO NA UVUVI

Posted on: August 8th, 2022

VYAMA VYA USHIRIKA VYATAKIWA KUWA MKOMBOZI WA WAKULIMA, WAFUGAJI NA WAVUVI

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amevitaka Vyama vya Ushirika vya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi nchini kuwa msaada katika kuleta maendeleo na sio kushiriki kushusha maendeleo ya wadau wa sekta hizo.

Naibu Waziri Ulega ameyasema hayo jana tarehe 07.08.2022 katika siku ya Mifugo na Uvuvi ya Maadhimisho ya Wiki ya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini kwenye Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, ambapo amesema lengo la kuanzishwa kwa ushirika ni kuwasaidia wanyonge kuwa na nguvu moja itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi.

Vyama vya Ushirika ni muhimu kwa wafugaji na wavuvi kwani vinasaidia kuwakutanisha pamoja ambapo wataweza kupata fursa mbalimbali zikiwemo za mikopo na bima. Wizara inaendelea kuwahamasisha wafugaji na wavuvi kujiunga kwenye vyama vya ushirika kwa kuwa ni njia ambayo itawafanya wawe na nguvu moja kwenye maamuzi ya biashara ya mazao yao.

Naibu Waziri Ulega pia amewataka viongozi wa Vyama vya Ushirika kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu kwani kumekuwepo na malalamiko mengi kwenye baadhi ya vyama kutokana na ukiukwaji wa taratibu za uendeshaji kitu kinachosababisha wakulima, wafugaji na wavuvi kuilalamikia serikali.

Vilevile ameendelea kuwasihi wananchi kutumia mazao yatokanayo na mifugo na uvuvi kwa kuwa ni muhimu katika kujenga na kuimarisha afya. Pia amewashauri watanzania kuendele kutumia bidhaa mbalimbali zinazotokana na zao la ngozi kama viatu, mikanda na mikoba kwa kuwa bidhaa hizo ni bora na zinazalishwa hapa nchini.

Naibu Waziri Ulega amewasihi wafugaji kuhakikisha wanavisha hereni za kielektroniki kwenye mifugo yao kama taratibu zinavyotaka kwa kuwa mfumo huo una faida kubwa. Serikali inaendelea na uboreshaji wa mazingira ya wafugaji kwa ujenzi wa majosho, malambo na uhamasishaji wa utunzaji wa nyanda za malisho na kilimo cha malisho ya mifugo ili wakati wa kiangazi wafugaji wasiweze kupata tabu. Pamoja na mambo mengine kwa mkoa wa Lindi, Wizara inajenga Malambo kwenye Kijiji cha Kimambi (Wilayani Liwale) na Matekwe (Wilayani Nachingwea) ili wafugaji waweze kupata maji ya kunyweshea mifugo yao.

Aidha, amesema Wizara hiyo inakusudia kuanza kutoa mikopo kwa vifaa kwa wavuvi ili waendeleze shughuli zao na hatimaye kuinuka kiuchumi, ambapo pia amesema zipo boti 250 za kisasa ambazo zitakopeshwa kwa wavuvi. Huku akibainisha kwamba kipindi kirefu wavuvi wamekuwa wakitumia zana duni za uvuvi na hivyo kuvua kwa kubahatisha lakini sasa serikali imedhamiria kumsaidia mvuvi kuhakikisha anakwenda kuvua eneo ambalo samaki wanapatikana.

Pia Naibu Waziri Ulega amewataka viongozi wa vijiji kuhakikisha wanasimamia Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ili maeneo yanayotengwa kwa ajili ya shughuli za mifugo zisiweze kuingiliwa na watumiaji wengine wa ardhi. Lakini pia amewasihi wafugaji kuto lisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima kwa kuwa hiyo ni moja ya chanzo cha migogoro na ikitokea tukio kama hilo serikali itachukua hatua.

”Wakulima na Wafugaji ni ndugu kwa kuwa wote wanategemeana, hivyo ni vyema kila mmoja akaiheshimu kazi anayoifanya mwenzake ili wote kwa pamoja waweze kuendelea na kujiingizia kipato kutokana na shughuli wanazofanya,” alisema Naibu Waziri Ulega

Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Mhe. Judith Nguli amesema kuwa kupitia elimu inayotolewa kwenye maonesho ya nanenane anaamini wakulima, wafugaji na wavuvi watakwenda kutumia mbinu za kisasa kwenye shughuli wanazofanya, kitu ambacho kitawasaidia kuongeza tija katika uzalishaji na biashara ya mazao hayo.

Kwa upande wake Dkt Hasan Mruttu Mkurugenzi Msaidizi Utafiti na Mafunzo amezishauri Halmashauri kuendelea kuwahamasisha wafugaji na wavuvi kujiunga kwenye vyama vya vyama vya ushirika ili viwasaidie katika kutetea maslai yao.

  1. Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo, Dkt. Erastus Mosha amewashukuru viongozi wa Kanda ya kusini kwa maandalizi mazuri waliyoyafanya kwa kuwa wakulima, wafugaji na wavuvi wanapata fursa kubwa kupitia maonesho hayo kukutana na wadau mbalimbali kwenye mnyororo wa thamani wa mazao yao.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.