Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira leo tarehe 17 Mei, 2025 amtembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi na kukutana na katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary @jirized kwa lengo ya kujitambulisha kisha kuanza ziara ya kukagua zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili kwenye vituo mbalimbali vya uandikishaji wapiga kura katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi na Mtama, mkoani Lindi.
Katibu Tawala Bi Zuwena Omary amesema kuwa elimu na hamasa ya uboreshaji wa taarifa awamu ya pili itaendelea kutolewa ili kika mwenye sifa na sababu ya kuhakiki na kuboreasha taarifa zake afanye hivyo .
Zoezi hilo ambalo lipo kwenye mzunguko wa pili linafanyika pamoja na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura.
Mikoa ya mzunguko wa pili ni pamoja na Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba ambapo zoezi hilo linafanyika kuanzia tarehe 16 Mei, 2025 hadi tarehe 22 Mei, 2025 na vituo vinafunguliwa saa 2:00 Asubuhi na kufungwa saa 12:00 Jioni.
@tumeyauchaguzi_tanzania
@ortamisemi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.