Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura Mkoani Lindi linatarajiwa kufanyika kwa kipindi cha muda wa siku saba kuanzia Januari 28 hadi February 3 2025 likihusisha uandikishaji wa wapigakura wapya pamoja na kutoa kadi mpya kwa wapigakura waliopoteza kadi au kuharibika.
Akizungumza katika Mkutano na Tume na Wadau wa Uchaguzi kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura, Bi. Giveness Aswile ameeleza kuwa kwa mujibu wa sensa ya Watu na Makazi 2022 Mkoa wa Lindi unatarajiwa kuandikisha wapigakura wapya 121187 sawa na 18% na kufanya idadi kamili ya wapigakura katika Mkoa wa Lindi kufikia watu 768641 ukilinganisha na uchaguzi wa mwaka 2020 uliokuwa na wapigakura 645644 huku Mkoa ukiwa unatarajiwa kuwa na vituo vya uboreshaji taarifa za wapigakura 1308, ikiwa ni ongezeko la vituo 70.
Akitoa hotuba yake, Makamu Mwenyekiti wa INEC, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mst) Mbarouk S. Mbarouk ameeleza kuwa uboreshaji wa daftari mwaka 2025 utatumia teknolojia ya BVR Kits zilizoboreshwa kwa kuwekwa program endeshi ya kisasa.
"Mfumo wa teknolojia hii ya BVR hutumika katika kumtambua mtu na kumtofautisha na mwingine kwa kuwa unahusisha uchukuaji wa alama za vidole vya mikono, picha na saini na kuhifadhiwa katika kanzidata ya wapigakura. Napenda kuwakumbusha wadau na wananchi kuwa kujiandikisha kwa mpigakura zaidi ya mara moja ni kosa la jinai kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 114(1) cha sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024" Ameeleza.
Vituo vya Uboreshaji wa Daftari la Wapigakura vinatarajia kuanza kufunguliwa kuanzia saa 2:00 asubui na kufungwa saa 12:00 jioni.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.