MKOA WA LINDI UPO SALAMA, WANANCHI WAKAPIGE KURA OKTOBA 29, 2025.
RC LINDI Katika hafla ya kukabidhi vitendea kazi kwa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Lindi, leo tarehe 24 Oktoba 2025, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack, amewahakikishia wananchi wa mkoa huo kuwa upo salama hakuna tishio lolote hasa kuelekea uchaguzi Mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
“Mpaka sasa mkoa wetu uko salama, kwahiyo nitumie nafasi hii pia kuwaomba wananchi wa mkoa wa Lindi tarehe 29 asubuhi mapema wakajitokeze kwenye vituo vilivyoandaliwa kwa ajili ya kupiga kura ya kumchagua rais, diwani pamoja na mbunge kwenye majimbo yao yaliyopo. Ambacho nataka kuwahakikishia wananchi wa mkoa wa Lindi ni kwamba Mkoa uko salama sana, uko tulivu sana,” amesema Mhe. Telack.
Aidha, Mhe. Telack amevitaka vyombo hivyo kuendelea kudumisha amani kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.