Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omari amewapongeza Walimu wa Mkoa wa Lindi kwa kazi na jitihada kubwa zinazofanyika katika kuinua ufaulu katika Mkoa wa Lindi katika pimaji mbalimbali za kitaifa ambapo katika Mitiani ya Taifa ya Kidato cha Sita Mkoa umefanikiwa kufaulisha wanafunzi kwa asilimia 100.
Bi. Zuwena ametoa pongezi hizo wakati wa kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mpango Mkakati wa Elimu kwa kipindi cha Januari hadi Juni, ambapo ameongeza kuwa ni muhimu kwa walimu kufuatilia mienendo ya wanafunzi wao hadi kipindi wanakaribia mitiani yao ya mwisho ili kubaini changamoto ndogondogo ambazo zinaweza kuwapelekea kutopata matokeo yaliyo bora zaidi hususan katika kipindi hiki ambacho Mkoa wa Lindi unaendelea kupunguza matokeo ya daraja la nne katika mitiani ya kidato cha sita.
Aidha, katika kuzidi kufikia malengo ya ufaulishaji wa wanafunzi, Katibu Tawala amewataka walimu kuendelea kuwasimamia wanafunzi kitaaluma na kimaadili ili kuwajengea uwezo na nidhamu katika masomo yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.