Rais Samia ametekeleza ahadi yake ya kutoa miche elfu 60 ya minazi kwa mkoa wa Lindi ikiwa Mkoa wa Lindi na Mtwara imepata miche laki Tano.
Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo kwa maafisa kilimo kutoka Wilaya sita za mkoa wa Lindi, Meneja wa kituo cha utafiti wa kilimo mikocheni(TARI) Dk.Fredy Tairo, amesema kuwa wananchi wa mkoa wa Lindi na Mtwara waliamua kumuomba Rais Samia miche ya zao la minazi kutokana na minazi iliyopo katika mikoa hiyo kuwa ya muda mrefu na imekuwa ikikauka kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kushambuliwa na wadudu.
Dk.Tairo amesema kuwa wastani wananchi milioni 14 wanatumia nazi ingawa uzalishaji wake umeshuka kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi yanayopelekea kuibuka kwa mahonjwa pamoja nakukosa elimu ya utunzaji wa minazi.
"Rais Samia ametoa miche ya minazi Laki tano kwa mkoa wa Lindi na Mtwara ambapo Mkoa wa Lindi unapata miche elfu 60. Miche hiyo ya minazi imetolewa kwasababu minazi mingi ya zamani inaathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabia ya nchi hivbyo miche ya. Minazi hiyo na elimu inayotolewa. Kwa maafisa ugani itakwenda kupunguza tatizo na kuongeza uzalishaji."Amesema Dk.Tairo
Kwa upande wake kaimu katibu Tawala uchumi na uzalishaji Ndugu Ramadhani Khatibu amesema kuwa Licha ya kuwepo kwa ukame, zipo sababu zingine zinazopelekea kushuka kwa hali ya uzalishaji wa zao hilo ikiwemo kukosekana kwa viwanda vidogo .
"Sisi mkoa wetu hauna viwanda vidogo vidogo, nandio maana zao la nazi linashuka kila wakati, kungekuwa na viwanda; nazi ingekuwa na thamani kubwa kwani tungeweza kupata mafuta ya kutosha ,vifuu vingetengenezwa urembo wa wanawake.
Ndugu Khatibu ametumia fursa hiyo kumshukuru sana Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutekeleza ahadi yake kwa wananchi wa Lindi na Mtwara.
Naye Ofisa kilimo wa Wilaya ya Nachingwea Bi. Huruma Chiamba amesema kuwa watakwenda kusimamia wakulima ipasavyo ili miche hiyo iweze kuleta tija katika uchumi binafsi naTaifa."Zao la nazi litakwenda kuwa na thamani kubwa kwa mikoa yetu ya kusini kwani tutakwenda kusimamia vizuri wakulima wetu na kuweza kuongeza thamani ya zao la nazi pamoja na kuongeza pato kwa wakulima wetu" Bi. Chiamba.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.