• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

MKOA WA LINDI WAZINDUA MKAKATI WA KUBORESHA ELIMU MSINGI NA SEKONDARI.

Posted on: January 16th, 2023

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Kanali Ahmed Abasi amefanya kikao cha mapitio ya tathmini ya uboreshaji wa elimu katika mkoa wa Lindi pamoja na kuzindua mkakati wa kuboresha elimu msingi na sekondari katika mkoa wa Lindi ambao ulizinduliwa kitaifa na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 4 Agosti, 2022.

Akizungumza katika kikao hicho kilichowakutanisha  wadau wa elimu pamoja na walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari katika mkoa wa Lindi, Kanali Abasi amesema kuwa mkakati huo umekuja muda mwafaka ambapo uboreshaji wa elimu msingi na sekondari unahitajika sana hivyo kawataka wasimamizi wote wa elimu kuhakikisha wanafunzi wote katika kila ngazi wanapata ujuzi, stadi na maarifa kama yalivyoelekezwa kwenye mihtasari ya mafunzo.

“Ninafahamu leo mtapitishana kwa karibu namna bora mtakavyokuwa mnatekeleza mikakati tuliyojiwekea katika kuhakikisha wanafunzi wanapata ujuzi unaotakiwa. Hii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanafunzi wote wanapomaliza darasa la kwanza wawe na stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu, wanafunzi wanapomaliza darasa la saba wawe na umahiri wa lugha ya kiingereza, wanafunzi wa ngazi za elimu ya msingi na sekondari kuwa na umahiri wa kila somo wanalofundishwa na walimu kwa ngazi husika” amesema.

Aidha, Kanali Abasi amewapongeza viongozi na wasimamizi wa elimu msingi na sekondari katika mkoa wa Lindi kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya katika kuboresha elimu na kuongeza ufaulu wa wanafunzi kwa ngazi ya mkoa na kuongeza “Ni matumaini yangu kuwa leo mtajipanga vizuri ili kuhakikisha mwaka huu 2023 tunaanza kivingine. Hakikisheni mnafanya tathmini kila mwezi na kujirekebisha kila inapobidi ili tutakapofika mwisho wa mwaka, sio tu wanafunzi wanafaulu bali pia wanafunzi wanakuwa na ujuzi na umahiri uliokusudiwa”

Mwalimu Suzan Nusu, Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Awali na Msingi  amesema lengo la kikao hiki ni kukumbushana na kuweka mikakati ya kuboresha elimu msingi na sekondari kimkoa na nchini kiujumla ambapo pia ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama tawala kinachoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.

“Ni matarajio yetu kuwa kikao kazi hiki kinaenda kuwajengea uwezo wa kutekeleza maagizo tunayoenda kupeana, lakini pia tunatarajia kikao hiki kuibua ari, kutiana shime na kupeana munkari wa kutekeleza majukumu, yan kila mmoja akitoka hapa ajue kuwa serikali inatambua mchango wake kila mmoja kwa nafasi yake, aidha tunazidi kuweka msisitizo katika matumizi ya vitabu vitatu vya miongozo ya elimu vilivyozinduliwa kwa lengo la kumpa mwalimu mwongozo wa ufundishaji”

Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Ndg. Ngusa Samike amesema katika mpango wa kuboresha sekta ya elimu mkoa umepokea jumla ya Tsh. 32,971,069,001.6  kutoka serikalini ikiwa na lengo la kupunguza tatzo la upungufu wa miundombinu ya madarasa, mazingira ya shule, madawati, meza, viti, nyumba za walimu, matundu ya vyoo, uendeshaji wa shule, ujenzi wa mabweni na ujenzi wa shule mpya.

“Kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 tulipokea Tsh. Billion 8,100,000,000 za kujenga madarasa 401 kwenye shule za sekondari na vituo shikizi. Katika program ya EP4R tumeletewa fedha Ths. Billioni 3,510,000,000 za ujenzi wa shule mpya 5 za msingi, vyumba vya madarasa 16, mabweni 10, mabwalo 4, maabara 5, nyumba za walimu 4 na ukarabati wa shule 1” ameongeza Katibu Tawala.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.