• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

MKUU WA MKOA LINDI ATANGAZA OPARESHENI KALI KWA WAFUGAJI WATUKUTU

Posted on: November 9th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ametangaza oparesheni hiyo jana jumanne katika kikao chake na wafugaji wa mkoa wa Lindi  kilichohudhuriwa na Viongozi wa CCM, Wakuu wa Wilaya, Mkuu wa Oparesheni na Mafunzo Tanzania, Kamati za Usalama za Mkoa na Wilaya,  mwakilishi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Wataalam wa mifugo.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Telack ametangaza kupambana vikali na wafugaji walioingia kinyemela katika Wilaya za Lindi bila kufuata taratibu na kusababisha migogoro na wakulima. 

Akizungumza kwa hisia kali, Mhe. Telack ameoneshwa kusikitishwa na vitendo viovu vinavyofanywa na wafugaji dhidi ya wakulima bila kujali utu wala hofu ya mungu.

“Kwenye ziara ya Waziri wa Mifugo, tulikuta watu zaidi ya saba wana vidonda vipya, wamekatwa vichwa, wameshonwa nyuzi mpaka kumi kwenye vichwa….ndugu zangu haiwezekani, Tanzania haiwezekani, hiyo Tanzania haipo…….. Wamama wanalalamika, yupo shambani amelima shamba lake anataka kwenda kuchuma mboga, mfugaji anamwambia chuma za leo tu halafu anaingiza mifugo kwenye shamba lake, halafu anamwambia mama kaa hapo ashuhudie anavyolisha mifugo kwenye shamba lake…haiwezekani.” Amesema.

Mhe. Telack amewataka wafugaji wote ambao hawana vibali mkoani Lindi waanze kuondoka mara moja kabla oparesheni ya kuwaondoa haijaanza. Pia amewataka wafugaji ambao wamekaa maeneo ambayo hawakupangiwa ikiwemo maeneo ya hifadhi za misitu waondoke mara moja huku akiwatahadharisha kuacha mapuuza.

“Nimesikia wakisema oparesheni wamezizoea, sasa oparesheni hizo ambazo zilifanyika na watu wengine sio hizi tutakazozifanya sasa…….watu wote ambao wameingia Lindi bila utaratibu ninasema nimetoa siku mbili tuanze kuswaga mifugo.”

Kwa upande wake Mkuu wa Oparesheni na Mafunzo Tanzania CP. Awadhi Juma akioneshwa kusikitishwa na vitendo vya kihalifu ikiwemo mauaji yanayofanywa na wafugaji, amesema jeshi la Polisi halitavumilia vitendo vya kibabe vinavyofanywa na wafugaji dhidi ya wakulima na kuendelea kuhatarisha amani.

“ Mkoa wa Lindi kuna mauaji ya watu 12 ambao ni wakulima……na baadhi ya waliofanya uhalifu bado hawajakamatwa………… Sisi kama Jeshi la Polisi, chombo ambacho kimepewa dhamana ya kuulinda usalama wa raia na mali zao hatuwezi kukubali…………Wale ambao hawatatekeleza maelekezo na kuondoka kwa hiari yao, tutaendesha oparesheni  kali mno hata kama hiyo mifugo ni ya kigogo wa namna gani tutahakikisha sheria inafuatwa.”

Kwa upande wao wafugaji wameeleza kuwa migogoro mingi inasababishwa na kukosekana  kwa miundombinu ya maji kwenye maeneo mengi, uingiaji wa mifugo kwa njia za magendo lakini pia wizi wa mifugo. Akizungumza mbele ya kikao, Katibu wa wafugaji kanda ya Kusini Ndg. Daudi Balele amesema kuwa kwa kipindi hiki cha kiangazi maeneo mengi mashamba hayajalimwa, migogoro mingi inasababishwa na wezi wa mifugo. “ Nachingwea na Liwale ni Wilaya ambazo zina matatizo makubwa….kumezuka na wimbi la majizi  ya mifugo ndio wanaogombana na wafugaji……………..unaanzaje kwenda kufyeka mifugo ambayo haina kosa…..kuna uvunjifu wa amani mkubwa mno.”

Oparesheni ya kuwaondoa wafugaji wavamizi mkoa wa Lindi inafanyika baada ya vitendo vya uvunjifu wa amani kati ya wakulima na wafugaji kushamili. Tangu kuingia kwa wafugaji mkoani Lindi kumeibuka migogoro inayosababisha mapigano kati ya wakulima na wafugaji ambayo yamekuwa yakigharimu maisha ya wananchi na wengine kujeruhiwa.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.