• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

MKUU WA MKOA WA LINDI AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU

Posted on: April 9th, 2023






Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack jumamosi ya tarehe 08 April 2023 amezindua Mpango Mkakati wa Elimu Kwa ajili ya maendeleo ya sekta hiyo Kwa mwaka 2023.

Mhe. Telack akizindua Mpango Mkakati huo kwenye mkutano uliofanyika katika kiwanja cha mpira cha Ilulu, Manispaa ya Lindi amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Walimu wamefanya kazi kubwa ya kupandisha ufaulu wa wanafunzi kwa ngazi za msingi, kidato cha nne na kidato cha sita. Mhe. Telack ameongeza kuwa Kwa matokeo ya darasa la saba, ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 86.3 mpaka kufikia asilimia 86.42 na kushika nafasi ya nne kitaifa. Kwa kidato cha nne wanafunzi waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu wameongezeka kutoka 2352 mwaka 2021 mpaka kufikia 2612 mwaka 2022. Kwa kidato cha sita , kwa kipindi cha miaka mitatu ufaulu umekuwa  kwa asilimia 100.

Mhe. Telack amewapongeza Walimu, wazazi na wadau wote kwa ushirikiano mzuri uliozaa matunda hayo mazuri kwa Mkoa na Taifa Kwa ujumla.

Pamoja na maendeleo mazuri yaliyofikiwa kwenye sekta ya elimu, Mhe. Telack amewataka wazazi kushiriki kikamilifu kwenye utoaji wa chakula kwa wanafunzi shuleni ili waweze kupata nguvu ya kuhudhuria masomo pamoja kuelewa wanachofundishwa darasani.

Ameongeza kuwa hali ya utoaji chakula shuleni bado hairidhishi ambapo Kwa Shule za Msingi utoaji wa chakula ni asilimia 60 Tu na upande wa Sekondari ni asilimia 80.

Katika kuhakikisha chakula kinapatikana kwa Shule zote, Mhe. Telack amezitaka Shule zote kuanzisha mashamba ya Shule ili kuzalisha mazao ya chakula.

Mhe. Telack ameongeza kuwa ili kufikia malengo yaliyowekwa kupitia Mpango Mkakati wa Mkoa, Walimu wahakikishe wanawafuatilia wanafunzi ili kujua changamoto zinazowasababisha washindwe kufikia malengo na kufanya vibaya kwenye masomo yao. Amesisitiza Walimu waendelee kusimamia nidhamu za wanafunzi ili kujenga kizazi Chenye maadili na kuweza kukabiliana na changamoto za mmomonyoko wa maadili Kwa wanafunzi na jamii nzima.

Mhe. Telack amewaasa Walimu kutizama adhabu za kuwapatia wanafunzi pale wanapokosea badala ya kuwafukuza Shule. Ameongeza kuwa kumfukuza Shule Mwanafunzi ni kumnyima haki yake ya msingi.

Awali akiwasilisha taarifa mbele ya mgeni rasmi, Afisa Elimu wa Mkoa wa Lindi Ndg. Joseph Mabeyo amesema kuwa Mpango Mkakati wa mwaka 2023 umeandaliwa kwa kuzingatia taratibu mbalimbali ikiwemo Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na marekebisho yake ya 10 ya mwaka 2002, Sera ya Elimu ya mwaka 2014, Nyaraka, miongozo na maelekezo ya Viongozi na Serikali.

Ndg. Mabeyo ameongeza kuwa Mpango Mkakati uliozinduliwa unalenga kutatua jumla ya changamoto 16 ikiwemo suala la utoaji wa chakula kwa wanafunzi pamoja na kusimamia maendeleo yao ikiwemo uwezo wa kusoma na kuandika kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga amewaomba Walimu kujipanga kikamilifu katika kuutekeleza Mpango Mkakati uliozinduliwa ili tofauti ionekane Kati ya Mkoa wa Lindi na mikoa mingine kupitia matokeo ya mitihani ya Taifa.

Aidha, pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa maendeleo ya elimu, Mhe. Telack alitoa zawadi mbalimbali kwa wadau wote wa elimu walioshiriki katika kufanikisha matokeo mazuri ya mitihani ya taifa kwa ngazi zote za elimu kwa mwaka 2022. 

 














ReplyForward






Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.