Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amekutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Norway Mhe. Andrea Motzfeldt Kravik na ujumbe wake akiwemo Balozi wa Norway Nchini Tanzania Mhe.Toni Tinnes pamoja Equinor na shell na wasimamizi wa mradi huo TPDC leo Januari 10,2025.
Telack amemueleza Naibu Waziri huyo wa Mambo ya nje wa Norway Kravik namna ambavyo maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kuchakata na kusindika Gesi asili (LNG) yalivyofanyika ikiwemo kulipa fidia wananchi wote ambao walikuwa na miliki ya maeneo hayo na uandaaji wa michoro ya utekelezaji wa mradi huo.
Kwa upande wake Naibu waziri wa Mambo ya Nje ya Norway Adreas Kravik amepongeza hatua ambayo Serikali ya Tanzania imefikia katika mradi huo ambapo mbali na kuona na kujiridhisha juu ya eneo utakapotekelezwa amewahakikishia wanakwenda kujiandaa na kushawishi kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo Mkubwa nchini Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Telack aliongozana ugeni huo hadi katika eneo la Likong’o Manispaa ya Lindi ambako unatarajiwa kutekelezajwa
Baadhi ya manufaa yanayotajwa katika mradi huo ni kuchochea ukuaji wa uchumi, kuongeza pato la Taifa , ajira na kuongeza uwezo wa Watanzania kitaaluma.
Aidha Kati ya miaka minne hadi sita ya ujenzi wa mradi huu kunatarajiwa kuwa na ajira 10,000 na baada ya kukamilika kwa ujenzi, ajira za kudumu zitakuwa 500.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.