• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan: Ongezeni jitihada katika kupambana na unyanyapaa kwa waadhirika wa UKIMWI.

Posted on: December 1st, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo leo akiwahutubia wananchi  kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika Mkoani Lindi katika uwanja wa michezo Ilulu, Manispaa ya Lindi.

Mhe. Rais amesema kuwa pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana wa washirika wa maendeleo mbalimbali katika kupambana na UKIMWI bado changamoto ya unyanyapaa kwa waadhirika haijafanyiwa kazi vizuri . Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa  kwa sasa kuna mkakati wa tatu wa kitaifa wa kupambana na janga la UKIMWI ambao utasaidia kuondoa unyanyapaa kwa waadhirika.

“Kuna jambo ambalo hatujalifanyia vizuri, nalo ni suala zima la unyanyapaa, bado lipo na ndio maana tumekuja na mikakati hiyo ili kuondosha huo unyanyapaa.”

“Safari tunayokwenda katika mkakati unaofuata ni kufikia malengo ya sifuri 3 ifikapo mwaka 2030 lakini kwa mpango wetu ni 2026 ni kutokomeza UKIMWI kwa kuwa na sifuri ya maambukizi mapya ya VVU, sifuri ya kifo na sifuri ya unyanyapaa.”

Mhe. Rais amesisitiza kuwa katika kufikia malengo ya kutekeleza wa mpango huu wa miaka 5 ni vyema kushirikiana kwa kuwa mpango huu ni wa sekta zote, sio mpango wa Wizara ya Afya pekee.  Mhe. Samia ameilekeza Wizara ya Afya, TACAIDS kwa kushirikiana na sekta zote na wadau wote wa mapambano dhidi ya UKIMWI na VVU kuweka mkazo zaidi katika kuweka jitihada na mikakati madhubuti  katika kuzuia maambukizi mapya, kuimarisha huduma za upimaji VVU  na matumizi ya ARV ili kutokomeza vifo vitokanavyo na UKIMWI,  kuweka mikakati ya kutokomeza ubaguzi na unyanyapaa kwa waadhirika, WAVIU.

Akimkaribisha Mhe. Rais kuzungumza na  wananchi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa jitihada mbalimbali zimeendelea kufanyika katika mapambano dhidi ya UKIMWI. Mhe. Majaliwa amesema katika kupambana na janga la UKIMWI mikakati mitatu imeendelea kutekelezwa, kwanza ni pamoja na utafiti wa viashiria vya hali ya VVU hapa nchini ambao ulizinduliwa mwezi septemba 2022. Ameongeza kuwa utafiti huu hufanyika kila baada ya miaka minne ambao utamalizika mwaka 2022/23 ukilenga kupima magongwa ya  VVU, homa ya ini B na C. Mkakati wa pili ni mkakati wa tatu wa taifa wa kuthibiti UKIMWI ambao utajuisha sekta zote, na tatu ni mfuko wa udhamini wa udhibiti UKIMWI  ambao utakuwa na vyanzo endelevu ili kuhakikisha serikali inakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha afua za sekta zote katika kudhibiti VVU na UKIMWI.

Akitoa salam za Wizara ya Afya kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (Mb), Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Godwin Mollel (Mb) ameeleza hali ya maambukizi kwa nchi nzima kuwa Tanzania inakadiliwa kuwa na waadhirika milioni 1.7 na jumla ya waadhirika milioni moja laki tano na thelathini wamekwisha fikiwa na kupatiwa huduma. Ameongeza kuwa jitihada zinaendelea mpaka kufikia 2026 lengo la kufikia 95,95,95 litatimia. i.e 95 ya kwanza ni kuwafikia waathirika, 95 ya pili ni kuhakikisha wanatumia dawa za kufubaza VVU na 95 ya tatu, waathirika wawe wamefubaza VVU. Mhe. Molle amesema mpaka sasa 92.5% ya waathirika wote wamekwisha fikiwa, 98.3% wamekwisha pata dawa za kufubaza VVU na 97% wamefubaza VVU.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amemshukuru Mhe. Rais kwa kuupatia  Mkoa wa Lindi fursa kubwa ya kuwa mwenyeji  wa Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kwa mwaka 2022. Mhe. Telack pamoja na shukrani hizo amemshukuru pia Mhe. Rais kwa kuupatia Mkoa wa Lindi jumla ya Tsh. Bilioni 26.8 kwa ajili ya kujenga na kuimarisha miundombinu na huduma za afya, kununua vifaa tiba na dawa.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.