Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary ambaye nidye mwenyekiti wa kamati ya Lishe Mkoa wa Lindi, ameongoza kamati hiyo kupitia na kujadili utekelezaji wa afu za lishe kwa kipindi cha April hadi Juni , 2025.
Katika kikao hicho, Mwenyekiti amewataka watalaamu wa sehemu, vitengo na Taasisi mbalimbali kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa kina ili jamii iwezekubadilika na kupokea ushauri wa kitaalamu wa kilimo bora, ulaji bora kuanzia maandalizi ya ujauzito, Utoto na umri mkubwa lengo kupata jamii yenye afya bora na uzalishaji.
Wito huo umeambatana na msisitizo ambao unazitaka shule zote kutekeleza agizo la kuwa na mashamba ya chakula ambayo yatasaidia wanafunzi kupata chakula shuleni.
Aidha, wananchi wanashauriwa kushirikisha maafisa mifugo kila wanapotaka kuchinja mnyama aidha kwa matumizi ya nyumbani au biashara kwa ajili ya kuchunguza afya ya mnyama huyo kabla ya kutumika . Lengo kuepusha mazingira ya maambukizi ya magonjwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu ikiwa mnyama atakuwa na ugonjwa ambao haujabainika na wataalamu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.