RC LINDI ARIDHISHWA NA HATUA YA UJENZI WA BANDARI YA UVUVI KILWA
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack ametembelea mradi wa ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Wilaya ya Kilwa Oktoba 15,2025 na kuridhishwa na hatua ya utekelezaji wa mradi huo. Kukamilika kwa bandari hiyo kutawezesha meli za uvuvi zinazovua katika ukanda wa uchumi wa Bahari ya Tanzania na bahari kuu kutia nanga na kushusha samaki wanaolengwa na wale wasiolengwa kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi. Aidha, amewataka wakandarasi na wadau wote wanaohusika kuharakisha ukamilishaji wa bandari hiyo ianze kutumika mapema ili kutoa fursa kwa wavuvi na wafanyabiashara kunufaika na huduma zitakazotolewa. Mhe. Telack pia amesisitiza umuhimu wa kuandaa mazingira mazuri ya amani na usalama katika eneo la bandari, kuhakikisha ulinzi wa watu na mali, hasa wakati shughuli za bandari zitakapokuwa zinaanza rasmi. Amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Wilaya ya Kilwa pamoja na wadau mbalimbali katika kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa viwango vinavyokidhi matarajio ya Serikali na wananchi wa Mkoa wa Lindi. Ikumbukwe kuwa uwepo wa bandari ya uvuvi kikwa utachochea uwekezaji katika ujenzi wa viwanda vya kuchakata samaki na miundombinu ya uhifadhi wa mazao ya uvuvi. Hivyo , uwekezaji huu, unaenda kuimarisha biashara ya mazao ya uvuvi kwenda nje ya nchi kautoka tani 40,721.53 zenye thamani ya Dola za marekeni Milioni 249.54 hadi tani 52,937.99 na kuchangia takribani asilimia 10 katika pato la Taifa ifikapo mwaka 2036.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.