Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Zainab Telack leo tarehe 17/12/2024 amezindua kituo cha polisi wilaya ya lindi.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi wa serikali na vyama vya siasa, viongozi wa dini, makampuni binafsi, maafsa, wakaguzi, askari wa vyeo mbalimbali na wananchi.
Akihutubia hadhira iliyohudhuria ufunguzi huo Mh. mkuu wa Mkoa amemshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Samia Suluhu Hassani kwa muda mfupi ambao amekuwepo madarakani kwa kulitazama jeshi la polisi hasa kwenye kuboresha miundombinu ya kufanyia kazi na pia miundombinu ya usafirishaji ndani ya jeshi la polisi.
Ametumia fursa hiyo kulipongeza jeshi la polisi kwa kazi kubwa ya kusimamia amani na kufanya mkoa wa Lindi kuwa wenye utulivu wakati wote.
Awali katika hotuba yake ya kumkaribisha mgeni rasmi kamanda wa polisi mkoa wa lindi Acp. John Imori alisema ujenzi wa kituo hicho daraja A ulianza Mwaka 2022 nakukamilika 2023 ambapo mkandarasi wa mradi huo alikuwa ni fundi mkuu wa kikosi cha Polisi cha ujenzi . Mradi huu umetumia kiasi cha Milioni mia tisa arobaini na nane laki tatu themanini na nne elfu mia tisa hamsini na moja (948,384,951/=)
Sambamba na ujenzi huo, Acp J. Omori alitaja miradi mingine ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya polisi vinayoendelea katika hatua mbalimbali ndani ya mkoa wa lindi. miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa kituo cha Polisi daraja c na nyumba mbili za makazi ya askari kwenye kata ya Nandagala wilaya ya Ruangwa Milioni 164, ujenzi wa kituo cha polisi daraja c kwenye kata Kibutuka wilaya ya Liwale wa Milioni 115, ujenzi wa kituo cha polisi daraja c kwenye kata ya Somanga wilaya Kilwa wenye thamani ya sh Milioni 115, Ujenzi wa kituo cha Polisi daraja c kata Tingi wilaya ya kilwa wenye thamani ya sh Milioni115, Ukarabati wa kituo cha Polisi kwenye kata ya Naipanga wilaya ya Nachingwea Milioni 52, ukarabati wa kituo cha Polisi Nanjilinji kwenye kata ya nanjilinji wilaya ya kilwa Milioni 15.
Aidha, Mhe. Telack ametumia jukwa hilo kuwaomba viongozi wa dini kuwaombea watoto ambao wapo katika hatari ya matendo ya ukataili wa kijinsia na mmomonyoko wa maadili.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.