RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU MKOA WA LINDI.
Katika kuhakikisha Mkoa wa Lindi unaendelea kuongeza ufaulu na viwango vya ufaulu Mhe. Telack amesisitiza kuhusu kufanya ufuatiliaji wa ufundishaji na ujifunzaji mashuleni kwa kuzingatia maelekezo ya Miongozo mitatu ya elimu yaliyozinduliwa Agosti, 2022, Mikataba ya utendaji kazi na maelekeo ya Mpango Mkakati wa Elimu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya kufanya tathmini na ufuatiliaji wa namna ya ufundishaji na ujifunzaji shuleni.
Maelekezo hayo yametolewa wakati wa hafla ya Utoaji tuzo za Ufaulu na Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Elimu Mkoani Lindi zilizofanyika Wilayani Ruangwa ambapo Mhe. Telack amewapongeza walimu, wanafunzi na wasimamizi wa sekta ya elimu kwa kuonyesha umahiri unaozidi kuuinua mkoa wa Lindi Kielimu.
"Haya si mafanikio ya bahati nasibu, bali ni matokeo ya kazi ya pamoja, mshikamano na nidhamu ya hali ya juu katika uongozi, usimamizi wa elimu na uwajibikaji wa kila mdau wa elimu hivyo tendo la utoaji wa tuzo ni motisha na kichocheo katika kuchagiza ufanisina utendaji kazi wenye kutoa matokeo chanya na kuthamini kazi nzuri mnayofanya, hongereni sana" Mhe. Telack.
Aidha, Mhe. Telack amesisitiza kuhusu umuhimu wa utoaji mashuleni kama nyenzo ya kumfanya mwanafunzi aweze kufanya vizuri zaidi kitaaluma pamoja na kuagiza walimu na maafisa elimu kusimamia shughuli za elimu ya kujitegemea (EK) ili kuwezesha wanafunzi kujifunza shughuli za mikono wakiwa shuleni.
Kwa kuzingatia kuwa mafanikio ya mwanafunzi unahusiana na nidhamu aliyonayo, Mhe. Telack amewataka walimu kusimamiza nidhamu na mienendo ya wanafunzi wawapo mashuleni ikiwa ni sambamba na kuhakikisha ufuatiliaji wa ufundishaji wa vipindi vya dini mashuleni.
"Naelekeza Wakuu wa shule za Msingi na Sekondari na walimu wote kuendelea kusimamia nidhamu za wanafunzi ipasavyo sambamba na kusimamia matumizi ya kipindi cha dini shuleni, wanafunzi wasimamiwe waweze kushiriki ibada kwa imani zao ili tujenge jamii yenye hofu ya Mungu na inayofata miongozo ya dini" Amesisitiza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.