• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

SIMAMIENI MRADI WA ZAHANATI UKAMILIKE KWA WAKATI

Posted on: April 14th, 2023

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg. Abdalla Shaib Kaim Leo Ijumaa  ametoa maagizo hayo katika Wilaya ya Kilwa muda mchache baada ya Mwenge wa Uhuru kufika Wilayani hapo.

Akizungumza na wananchi kwenye  mradi wa ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha mirumba, Kata ya Kiranjeranje Wilaya ya Kilwa baada ya Mwenge wa Uhuru kufanya ukaguzi wa mradi huo, Ndg. Kaim ametoa maagizo kwa viongozi wote wa Wilaya kusimamia kwa ukamilifu ujenzi wa mradi huo ili urahisishe upatikanaji wa huduma za afya kwa kijiji cha mirumba na vijiji jirani.

Ndg. Kaim amesisitiza kuwa wananchi wanasubiri kunufaika na adhima ya Mhe. Rais ya kuimarisha miundombinu pamoja na kutoa huduma bora kwa jamii.

Ndg. Kaim amewapongeza wananchi wa kijiji cha mirumba kwa kuonesha uzalendo wa hali ya juu kwa kujitoa na kushirikiana kuanzisha ujenzi wa Zahanati yao.

Hivyo, Ndg. Kaim ametoa wito kwa wananchi wote kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuleta maendeleo kwa kujitoa na kujisimamia.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Christopher Ngubiagai amesema kuwa ujenzi wa mradi wa Zahanati ya kijiji cha mirumba ulianzishwa na wananchi wenyewe ili kuondokana na changamoto ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Hivyo baada ya kuanzisha ujenzi huo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha taktibani milioni 50 ili kukamilisha ujenzi wa Zahanati hiyo.

Mhe. Ngubiagai ameongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekwisha tenga kiasi cha fedha takribani milioni 200 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vitakavyotumika baada ya ujenzi wa Zahanati hiyo kumalizika.

Aidha, Mbunge wa Jimbo la Kilwa kusini, Mhe. Ally Kassinge amemshukuru Rais kwa kusikia Kilio cha wananchi wa kijiji cha mirumba na kuchukua hatua za dhati katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa kijiji hicho na vijiji jirani.

Mhe. Kassinge ameiomba Serikali kujiandaa kupeleka wataalam watakao hudumu katika Zahanati hiyo pamoja na mahitaji yote ikiwemo vifaa vya matibabu pamoja na dawa.

Mhe. Kassinge amewaahidi wananchi wa Jimbo lake kuwa ataendelea kutumia nafasi ya uwakikishi wao bungeni Kuomba fedha zaidi Kwa ajili ya maendeleo ya kijiji cha mirumba na Kilwa kusini Kwa ujumla.



Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.