LINDI: VIONGOZI WATAKIWA KUWA NA WELEDI KATIKA UTEKELEZAJI WA MPANGO JUMUISHI WA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Zainab Telack amewasihi viongozi wa wilaya na mkoa kuzingatia Weledi katika utekelezaji wa Mpango jumuishi wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii kwa Mkao wa Lindi .
Mhe. Ndemanga ameyasema hayo leo Juni 10, 2024 katika utambulisho wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha uuguzi Lindi na kuhudhuriwa na viongozi wa Wilaya na Mkoa .
“Niwakumbushe mambo mawili ya msingi, moja tunapaswa kuwa na weledi katika utekelezaji wa mpango huu, kwani yapo mambo mengi ambayo yanaweza kuibuka wakati wa utekelezaji hasa katika zoezi la kuchagua watoa huduma ambao kimsingi wanachaguliwa na wanajamii wenyewe “ Mhe. Ndemanga.
Mhe. Ndemanga ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wataalam ngazi ya wilaya na mkoa juu ya umuhimu wa kutunza kumbukumbu vizuri, ambazo zinasaidia sana kuondoa sintofahamu wakati wa utekelezaji na baada ya utekelezaji wa kuwapata watoa huduma ngazi ya jamii na shughuli zingine muhimu za kiutendaji.
“ Bila shaka mnafahamu juu ya umuhimu wa kumbukumbu, hivyo katika zoezi hili tunapaswa kuzingatia kuweka kumbukumbu sawa kama ambavyo mazoezi mengine yalivyofanyika vizuri “
Kwa upande wake Bi. Orsolina Tolage ambaye ni Afisa progamu wa mpango wa Huduma za Afya ngazi ya jamii kutoka Wizara ya Afya Idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya Kwa Umma ameeleza malengo ya mpango huo pamoja na kuzuia magonjwa yasiyo ambukiza kama vile Malaria, Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora pamoja na magonjwa yanayotokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Na Afisa Maendeleo ya Jamii idara ya Serikali za Mitaa Ofisi ya Rais –TAMISEMI Ndugu Jeremiah Mwambange akieleza muongozo wa utaratibu wa kuwapata wahudumu wa Afya ngazi ya jamii amesema kuwa, jamii ndiyo yenye jukumu la kumchagua mhudumu wa Afya ngazi ya jamii kadri watakavyoona anafaa kuwahudumia kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa .
Serikali imeweka utaratibu wa kuwapa mafunzo ya kuwajengea uwezo wahudumu tajwa kupitia vyuo vya Afya vya kati na hatimaye kuwawezesha kutekeleza majukumu ngazi ya jamii kwa kuwapa vitendea kazi na motisha.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.