WADAU WAMIMINIKA KUTEMBELEA BANDA LA MKOA WA LINDI.
Wadau mbalimbali na watumishi kutoka Taasisi na Sekta mbalinbali wamiminika kutembela banda la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi wiki ya Maadhimisho ya Utumishi wa Umma kitaifa 2025 viwanja vya Chinangali Dodoma..
Banda la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi likijumuisha halmashauri zake sita zimeshiriki maadhimisho hayo kwanamna ya kipekee ambapo zimekuja na mifumo rafiki ya kutoa huduma kwa wananchi kwa njia rais kama vile mfumo jumuishi wa kutoa huduma kwa wananchi (One Stop Centre ), Kadi-Alama, fursa za uwekezaji Mkoa wa Lindi, mfumo wa kidigitali wa usimamizi rasilimali watu wa ndani na ufuatiliaji wa mfumo wa hewa ukaa unaotekelezwa halmashauri ya Mtama .
Hayo ni baadhi ya mambo yanayowavutia wengi kuja kujifunza katika banda la Mkoa wa Lindi.
Unakaribishwa sana haujachelewa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.