• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

MKUU WA MKOA WA LINDI AWATAKA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUDUMISHA AMANI.

Posted on: June 19th, 2021

Akizungumza kwenye mkutano uliojumuisha wakulima na wafugaji uliofanyika jana tarehe 18 Juni 2021 eneo la shule ya msingi Nangurukuru iliyopo wilayani Kilwa, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab R. Terack ameyataka makundi hayo mawili kudumisha amani katika shughuli zao za maerndeleo. Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wataalam mbalimbali wa serikali ziliibuliwa hoja nyingi za migogoro zikielekezwa pande zote mbili ikiwemo kuuawa kwa mfugaji kijiji cha Njinjo, Kilwa na kuuawa mifugo.

Mgogoro mkubwa ulielekezwa kwa wafugaji wakituhumiwa kulisha mazao ya wakulima na kusababisha hasara kubwa ambayo hata hivyo malipo yake huwa hayaendani na dhamani ya mazao husika. Kundi la wakulima limeonekana kuchoshwa na vitendo vya wafugaji hao kuwasababishia hasara lakini wanapohoji huambulia kipigo kutoka kwa wafugaji. "Ki ukweli sie hatuwawezi kwa sababu wao wanatumia fimbo na sime." mmoja wa wakulima alieleza.

Mfugaji Donald Robert alieleza mbele ya mkutano kuwa chanzo kikubwa cha migogoro ya wafugaji na wakulima ni uhaba wa maji hasa kipindi cha kiangazi. Aliendelea kueleza kuwa, kipindi cha kiangazi wafugaji wengi huelekea mto mbwemkulu ambako hukutana na shughuli za kilimo cha umwagiliaji jambo ambalo huibuia migogoro. Pamoja na ukame bwana Donald aliongezea kuwa sababu nyingine ya wafugaji kuhama hama ni vitendo vya uchomaji moto kiholela kitendo ambacho huharibu malisho. Mfugaji huyo alienda mbali kwa kuiomba Serikali kutengeneza miundombinu ya maji kwa ajili ya mifugo na kuondoa changamoto zinazojitokeza.

Mhe. Zainab R. Telack amewataka wafugaji na wakulima kufanya shughuli zao kwa maslahi ya uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla huku wakizingatia taratibu zilizowekwa na serikali. Mhe. Mkuu wa Mkoa alionesha masikitiko yake kuhusiana na vyanzo vya migogoro inayojitokeza hasa vitendo vya rushwa kwa viongozi wa vijiji, uchomaji moto wa misitu na pembezoni mwa barabara. Katika kuhakikisha migogoro inakoma, Mkuu wa Mkoa amewataka wafugaji kuchimba malambo ya kunyweshea mifugo yao na kuacha vitendo vya kuhama hama huku akipiga marufuku uingizaji wa mifugo mipya ndani ya mkoa. "Sitaki mifugo mipya, sitaki wafugaji wapya na wafugaji waliohamia mkoa wa pwani wasirudi tena."  alisema akimuelekeza Kamanda wa Polisi Wilaya na Afisa Usalama Wilaya kusimamia hilo.

Mkuu wa Mkoa amewataka watendaji wote kuwajibika kwa kuchukua hatua kwa vitendo vinavyochochea migogoro kwenye jamii. Aliwataka viongozi wa vijiji kukomesha uchomaji moto kiholela kwa kuwachukulia hatua wahusika na kiongozi atakaeshindwa kudhibiti suala la moto Kamanda wa Polisi Wilaya ashughulike nae.

Makundi ya wafugaji na wakulima ni makundi muhimu sana kwenye uchumi na maendeleo ya mkoa, hivyo ni lazima kwa serikali kuchukua hatua pale ambapo kunahitaji nguvu eidha ya kimaendeleo au kuweka mambo sawa. Mkuu wa Mkoa wa Lindi ameendelea na ratiba yake ya kukutana na kuzungumza na makundi mbalimbali ndani ya mkoa wake.

 

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA BUNGE YA LAAC YAITAKA SUMA JKT KUONGEZA NGUVU KATIKA UJENZI WA OFISI YA HALMASHAURI YA MTAMA

    March 22, 2023
  • DKT. MAHERA AZINDUA MAFUNZO YA MFUMO MSHITIRI.

    March 22, 2023
  • NDG. NGUSA SAMIKE AKABIDHI OFISI KWA BI. ZUWENA OMARY.

    March 20, 2023
  • KAMATI YA BUNGE YASISITIZA UJENZI WA MRADI WA BANDARI YA UVUVI UMALIZIKE KWA WAKATI

    March 19, 2023
  • tazama zote

Video

Zambi aagiza kampuni za kukopesha fedha zichukuliwe hatua.
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.