Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa March 06, 2025 amegawa majiko ya gesi kwa wanawake zaidi ya 3000 ili kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais za matumizi ya nishati safi na utunzaji wa Mazingira.
Mitungi hiyo imeuzwa kwa bei ya ruzuku ya Shilingi 19,500 . Wanawake hao wamechangia kiasi hicho cha fedha na tayari zaidi ya Milion 40 zimeshakusanywa na kulipwa kwa kampuni ya Taifa Gas kwa ajili ya majiko hayo .
Siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 8 ya mwezi March kila mwaka kumefanyika makongamano mbalimbali nchini ambapo leo March 6, 2025 ni zamu ya kongamano hilo la kanda ya kisini linalofanyika Wilayani Nachingwea katika Viwanja vya Maegesho ya malori.
Moja ya ajenda katika makongomano haya ni uhamasishaji wa Matumizi ya nishati safi na utunzaji wa Mazingira.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.