• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Watumishi watakao kwamisha zoezi la upigaji chapa kuchukuliwa hatua.

Posted on: January 9th, 2018

Watumishi watakao kwamisha zoezi la upigaji chapa mifugo kuchukuliwa hatua.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega ameziagia halmashauri za mkoa wa Lindi kuhakikisha wanatekeleza agizo la upigaji chapa ng’ombe na watumishi watakao kwamisha zoezi hili watachukuliwa hatua.

Mhe. Ulega aliyasema hayo baada ya kukuta utekelezaji wa agizo la upigaji chapa mifugo upo chini huku halmashauri ya Kilwa ikiwa bado haijaanza kutekeleza. Mkoa wa Lindi una jumla ya ng’ombe 61,198 ambapo mpaka Mhe. Waziri anapita ng’ombe 8,545 walikuwa wameshapigwa chapa.

“Zoezi la upigaji chapa mifugo lipo kisheria na ni agizo alilolitoa Mhe. Rais hivyo kiongozi au mtumishi yoyote atakaye kwamisha utekelezaji wa agizo hili atachukuliwa hatua kali, hivyo niwatake viongozi na wataalam kuhakikisha kabla au ifikapo tarehe 31 January, 2018 zoezi hili liwe limekamilika”, alisema Mhe. Ulega.

Aidha, Mhe. Ulega aliwaagiza maafisa mifugo kwenda kwa wafugaji kutoa elimu ya ufugaji bora na matumizi ya mbegu bora zinazozalishwa katika kituo cha mbegu za uhamilishaji kilichopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Pia aliwaeleza maafisa mifugo kupitia upya takwimu za  upigaji chapa na kuhakikisha takwimu sahihi zinapelekwa wizarani.

Katika ziara yake hii, Mhe. Ulega alikutana na wavuvi na wachuuzi wa samaki katika soko la samaki la manispaa ya Lindi ambapo aliuagiza uongozi wa Manispaa ya Lindi kuhakikisha wanatoza ushuru wa samaki kwa asilimia tatu badala ya tano wanazotoza sasa.

Pia aliwaagiza viongozi wa manispaa kufanya mazungumzo na mamlaka ya bandari ili kuwaomba sehemu ya eneo kwa ajili ya ujenzi wa soko ambapo soko lililopo sasa halifai na lilijengwa toka wakati wa mkoloni. Vilevile aliwashauri waendelee kuwashirikisha wavuvi katika maamuzi mbalimbali wanayofanya yanayowahusu.

Awali akitoa taarifa ya Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi alimueleza Waziri kuwa Mkoa wa Lindi unaendelea kupambana na uvuvi haramu licha ya changamoto zilizopo katika kupambana na wavuvi haramu zikiwepo za uhaba wa vifaa na fedha ambapo ameiomba wizara kuangalia uwezekano wa kusaidia hasa upatikanaji wa boti.

Vilevile Mhe. Zambi alisema kuwa mkoa unaendelea kutatua migogoro iliyopo kati ya wafugaji na wakulima na ile ya mipaka.  Na kwamba mkoa utasimamia utekelezaji wa agizo la serikali la upigaji chapa mifugo kwa kuendelea kuwasimamia watendaji katika halmashauri.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.