SIDO katika kuwawezesha Wajasiriamali kukua na kujiendeleza katika uzalishaji bidhaa bora na utoaji wa huduma zao, wamekuwa na utaratibu wa kuandaa na kuratibu maonesho kila mwaka ambayo yamekuwa yakifanyika Kikanda.
Kupitia maonesho haya Wajasiriamali wamekuwa wakipata fursa ya kuonyesha kazi mbalimbali wanazozifanya ikiwa ni pamoja na kupata elimu na njia bora na za kisasa zinazowasaidia kuimarika katika uzalishaji na utoaji huduma.
Kanda ya Kusini na Mashariki inajumuisha Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Morogoro, Mtwara na Pwani. Ambapo kwa mwaka huu 2017 maonesho hayo yatafanyika Mkoani Lindi kuanzia tarehe 6 Novemba, 2017 hadi tarehe 12 Novemba, 2017 katika Uwanja wa Ilulu – Manispaa ya Lindi.
Tafadhali unaombwa upatapo ujumbe huu uwajulishe na wengine. Aidha, Wajasiriamali, Wafayabiashara, Taasisi mbalimbali, Wakulima na wananchi kwa ujumla maombwa kushiriki kwa wingi kwani hii ni fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yatakayokuwa yakionyeshwa.
Karibuni sana.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.