• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Huduma za Elimu

SEKTA YA ELIMU 

Mkoa wa Lindi wenye halmashauri 6 unazo taasisi mbalimbali za elimu zilizoanzishwa na serikali kwa lengo la kujenga taifa la watu thabiti, wenye misingi bora ya malezi, maadili, ujuzi, umahiri na uwezo wa kujitegemea katika dunia ya maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia (Sera ya Elimu na Mafunzo 2014).

Taasisi zenye dhamana ya utoaji elimu zilizopo katika Mkoa wa Lindi ni shule za msingi 498, shule za sekondari 122, chuo cha ualimu 1, vyuo vya maendeleo ya jamii 2, chuo cha VETA 1, chuo kikuu huria 1, taasisi ya elimu ya watu wazima 1, vituo vya ufundi stadi 14 na shule zenye mkondo maalum 6 na vituo vya MEMKWA 49. Pamoja na taasisi zilizotajwa kuna shule shikizi (satellite schools) 44 ambapo kila halmashauri ina shule za namna hiyo ambazo baadaye zitakuwa shule kamili.

TAARIFA ZA WANAFUNZI

Mkoa una jumla ya wanafunzi wa shule za msingi (darasa la I – VII) 202,762 wakiwemo wavulana 100,807 na wasichana 101,955. Kwa upande wa elimu ya sekondari wanafunzi waliopo ni 29,222 wakiwemo wavulana 14,864 na wasichana 14,358. Wanafunzi waliopangwa kujiunga kidato cha tano walikuwa 1,462 na walioripoti mpaka tarehe 18 Septemba, 2017 ni 1002. Hivyo, wanafunzi 460 hawakuripoti kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kubadilishiwa shule na wengine kujiunga na shule za binafsi.

Taarifa ya uandikishaji kwa mwaka 2017, kwa wanafunzi wa awali maoteo yalikuwa 29,920 (wav 14,828 na was 15,092), uandikishaji halisi ni 29,567 sawa na asilimia 99 (wav 14,524 na was 15,043). Wanafunzi wa darasa la kwanza maoteo 28,667 (wav 14,495 na was 14,172) uandikishaji halisi ni wanafunzi 36,246 sawa na asilimia 126.4 (wav 18,527 na was 17,719.

TAARIFA ZA WALIMU

 Ili ufundishaji na ujifunzaji uwe fanisi na wenye matokeo chanya kunahitajika pawepo na walimu wenye umahiri kwa ajili ya kutoa maarifa kwa wanafunzi waliopo. Mahitaji ya walimu kwa elimu ya msingi ni 5,104, walimu waliopo ni 3,721 na upungufu ni 1,383. Katika elimu ya sekondari upungufu wa walimu upo kwa walimu wa sayansi ambapo mahitaji halisi ni walimu 716, waliopo 243 na upungufu ni walimu 473   ambao ni sawa na 66.1%.

Katika jitihada za serikali za kuajiri walimu wapya, mkoa ulipangiwa walimu 103 wa sayansi awamu ya kwanza mwezi Aprili, 2017 na walioripoti ni walimu 96, walimu 7 hawakuripoti. Awamu ya pili mkoa ulipangiwa walimu 17 wa sayansi na hisabati na walioripoti ni walimu 8 na wasioripoti ni walimu 9. Mkoa hauna upungufu wa walimu wa masomo ya sanaa.

MIUNDOMBINU YA SHULE ILIYOPO

Miundombinu ni eneo muhimu sana katika kufanikisha suala zima la ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi. Katika elimu ya msingi mahitaji ya vyumba vya madarasa ni 4,908 na vilivyopo ni 3,101 na upungufu ni 1,804. Kwa upande wa nyumba za walimu mahitaji ni nyumba 4,262 zilizopo 1,270 na upungufu 2,993.

Kwa upande wa elimu ya sekondari kuna upungufu wa miundombinu kama ifuatavyo: mahitaji ya vyumba vya madarasa 833, vilivyopo 800 na upungufu 33, nyumba za walimu mahitaji ni 1,628, zilizopo 390, upungufu 1,238, vyumba vya maabara mahitaji ni 345 vilivyopo 114 na upungufu 231.  Aidha, katika matundu ya vyoo pia kumekuwa na upungufu mkubwa ukilinganisha na idadi ya wanafunzi waliopo kwa elimu ya msingi na sekondari.

MIRADI INAYOYOTEKELEZWA KATIKA MKOA  

Mkoa umekuwa ukitekeleza miradi/programu mbalimbali ikiwemo EQUIP- Tanzania katika halmashauri zote 6. Mpaka mwezi Agosti, 2017 kiasi cha Tsh. 8,458,143,629 kilipokelewa katika halmashauri za mkoa huu kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za program ya Equip-T. Programu ya LANES inatekelezwa katika halmashauri ya Wilaya ya Liwale (shule shikizi 10) na ikihusika na vituo vya MEMKWA kwa halmashauri 6. Pia miradi chini ya mpango wa EP4R inayohusika na fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mkoa umekuwa ukisimamia kwa karibu kuhakikisha dhima ya serikali inafikiwa.

UENDESHAJI WA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MWAKA 2017

Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) mwaka 2017 umefanyika kuanzia tarehe 6 na 7 Septemba, 2017 nchini kote. Kwa mkoa wa Lindi mtihani huu umefanyika katika shule 480 zenye jumla ya wanafunzi 17,519 wakiwemo wavulana 8,117 na wasichana 9,402 katika halmashauri 6 za mkoa wa Lindi. Aidha, mtihani huo ulifanyika katika mazingira ya utulivu, amani na usalama katika halmashauri zote.

TAARIFA ZA WATAHINIWA

Waliosajiliwa na waliofanya Mtihani

Jumla ya Wanafunzi 26,804 waliandikishwa kuanza darasa la I mwaka 2011, wanafunzi 17,519 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2017. Aidha, wanafunzi 17,392 (99.3%) walifanya Mtihani na wanafunzi 127 (0.7%) hawakufanya Mtihani huo kutokana na sababu mbalimbalikama inavyooneshwa katika jedwali na 1 na 2.

JEDWALI NA 1: MCHANGANUO WA WANAFUNZI WALIOFANYA MTIHANI  

Halmashauri
WALIOANDIKISHWA 2011
WALIOSAJILIWA 
WALIOFANYA MTIHANI
WV
WS
JML
WV
WS
JML
WV
WS
JML
%
Kilwa
3080
3050
6130
1931
2107
4038
1901
2078
3979
98.5
Lindi
2974
3303
6277
1629
2010
3639
1614
1993
3607
99.1
Lindi Manispaa
1006
1036
2042
729
815
1544
729
813
1542
99.9
Liwale
1452
1497
2949
1031
1169
2200
1026
1167
2195
99.6
Nachingwea
2617
2673
5290
1705
1894
3599
1696
1883
3579
99.4
Ruangwa
2085
2031
4116
1092
1407
2499
1086
1404
2490
99.6
JUMLA
13214
13590
26804
8117
9402
17519
8052
9338
17392
99.3

 

JEDWALI NA  2: MCHANGANUO WA WANAFUNZI WASIOFANYA MTIHANI  

Halmashauri
UTORO
VIFO
UGONJWA
SABABU NYINGINE
JUMLA
WV
WS
JML
WV
WS
JML
WV
WS
JML
WV
WS
JML
WV
WS
JML
Kilwa
27
19
46
1
1
2
2
2
4
0
7
7
30
29
59
Lindi
15
10
25
0
0
0
0
1
1
0
6
6
15
17
32
Lindi Manispaa
0
1
1
0
0
0
0
1
1
0
0
0
0
0
0
Liwale
4
2
6
1
0
1
0
0
0
0
0
0
5
2
7
Nachingwea
8
8
16
1
0
1
0
3
3
0
0
0
9
11
20
Ruangwa
3
3
6
3
0
3
0
0
0
0
0
0
6
3
9
JUMLA
57
43
100
6
1
7
2
7
9
0
13
13
65
62
127

Aidha, kwa mwaka 2017, Mkoa wa Lindi una jumla ya Wanafunzi 35 wakiwemo wavulana 17 na wasichana 18 ambao hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu waliofanya mtihani huu.

MAANDALIZI YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) MWAKA 2017

Mkoa umeendelea na maandalizi ya kufanyika kwa mtihani huo kwa kuendelea kusimamia ufundishaji na ujifunzaji katika ngazi ya shule kwa kila mwalimu. Walimu wakuu, waratibu elimu kata, wakaguzi na maafisa elimu ngazi ya wilaya wamekuwa wakisisitizwa kusimamia na kuhakikisha kazi ya ufundishaji na ujifunzaji inafanyika kikamilifu. Pia mkoa umeendesha mtihani wa dhihaki kwa shule zote za sekondari za serikali na zisizo za serikali na kutoa matokeo. Katika mtihani huo watahiniwa 3,878 kati ya watahiniwa waliosajiliwa 4,010 walifanya matihani.

Matokeo ya mtihani huo yanaonesha ufaulu wa daraja I – III ni watahiniwa 636 (16.4%), daraja la IV ni watahiniwa 2187 (56.4%) na daraja la 0 wamepata watahiniwa 1050 (27.1%). Halmashauri pia zimekuwa na mitihani inayoendeshwa na kusimamiwa vyema ikiwa ni jitihada za kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya mtihani wa kidato cha nne utakaofanyika mwezi Novemba mwaka 2017 nchini kote. Jitihada zinazofanyika kwa kidato cha nne pia zimekuwa zikisisitizwa kufanyika kwa vidato vyote ngazi ya shule.

MAANDALIZI YA WANAFUNZI KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2018

Mkoa wa Lindi wenye jumla ya shule za sekondari 116 zilizo za serikali unatarajia kupokea wanafunzi 17,392 (99.3%) wa kidato cha kwanza mwaka 2018. Idadi hiyo ya wanafunzi ndio waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) mwaka 2017. Hivyo basi, vyumba vya madarasa vitakavyohitajika kwa ajili ya wanafunzi hao ni 435 ikilinganishwa na vyumba 246 vilivyohitajika mwaka 2017 kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza wapatao 9,879 (65.16%) waliofaulu. Ili kuepukana na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa ni wajibu wa kila halmashauri kufanya maandalizi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mapema kabla ya zoezi la uchaguzi wa wanafunzi hao halijafanyika.

Mwezi Januari, 2017 halmashauri ya Kilwa (shule ya sekondari Kilwa Kivinje, Ali Mchumo, Kiranjeranje na Mpunyule) na halmashauri ya Ruangwa (shule ya sekondari Ruangwa, Chinongwe, Mnacho, Namichinga na Hawa Mchopa) zilikuwa na miundombinu pungufu iliyopelekea wanafunzi waliofaulu kubaki bila kupangwa. Hivyo, ni jukumu la kila halmashauri kujiandaa kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi hao ili isije ikajitokeza wakati wa zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 wanafaunzi wanabaki bila kupangwa katika shule husika kwa kukosa vyumba vya madarasa.

CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA ELIMU

Mkoa wa Lindi katika utekelezaji wa kazi za Sekta ya elimu unakumbana na changamoto mbalimbali miongoni mwa changamoto hizi ni: -

  1. Upungufu miundombinu na samani muhimu katika shule za msingi na Sekondari.
  2. Mwitikio mdogo wa wazazi/jamii kuwekeza katika sekta ya elimu kwa watoto wao kwa kuchangia na kugharamia elimu ya watoto wao.
  3. Usimamizi na ufuatiliaji hafifu wa wazazi/walezi katika mchakato wa kujifunza kwa watoto wao. Watoto wengi kuishi na kulelewa bila wazazi wao. Mfano: Manispaa ya Lindi kati ya wanafunzi 2,807 wa darasa la VII ni wanafunzi 562 tu (20.02%) ndiyo wanalelewa na wazazi wote wawili, aidha, kati ya wanafunzi wote 13,235 ni wanafunzi 5,824 sawa na 44.0% wanaokaa kwa wazazi wao wote wawili (utafiti: Feb. 2016).
  4. Ushiriki mdogo wa wazazi/walezi katika kudhibiti nidhamu za watoto wao na hivyo kusababisha wanafunzi kujiingiza kwenye makundi mbalimbali yasio na tija
  5. Upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.

MIKAKATI YA KUKABILI CHANGAMOTO KATIKA SEKTA YA ELIMU NA KUINUA TAALUMA KATIKA MKOA 

Baadhi ya mikakati ya kukabili changamoto za sekta ya elimu katika mkoa ni pamoja na;

  1. Kuendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa kujenga madarasa, vyoo, nyumba za walimu, maabara na kutengeneza madawati na samani kwa kushirikisha Serikali kuu, Halmashauri, wananchi na wahisani.
  2. Kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji ngazi za shule, kata, wilaya na mkoa na kuchukua hatua za kinidhamu kwa wote wanaokiuka maadili ya kazi.
  3. Kuendelea kurekebisha ikama ya walimu kwa kuzingatia mahitaji ya kila shule.
  4. Kuendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii kuthamini na kushiriki kusimamia na kufuatilia mchakato wa ujifunzaji kwa watoto wao na kuchangia nguvu kazi na rasilimali zingine za kuimarisha shule katika maeneo yao.
  5. Wilaya zote kuhakikisha wanafunzi wanaofaulu kuingia kidato cha I kila mwaka na wanaoandikishwa darasa la I wanafuatiliwa na wanasimamiwa kuhudhuria shule wakati wote wa masomo.
  6. Kuendelea kutoa mafunzo kazini kwa walimu ya kumudu stadi za KKK kwa wanafunzi wa darasa I & II na kuhakikisha watoto wote wanaoingia darasa la III kila mwaka wanamudu stadi za KKK.


Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.