• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Mifugo

HALI YA UFUGAJI MKOA WA LINDI

Mkoa wa Lindi kihistoria sio wa kiufugaji, wafugaji wachache waliopo hufuga zaidi mbuzi, kondoo, kuku, bata, kanga, njiwa na ng’ombe kwa uchache sana. Mara nyingi hutumiwa kwa kitoweo, shughuli za biashara, kimila na utamaduni. Hivyo, Mkoa wa Lindi una mifugo michache ukilinganisha na Mikoa mingine ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Nyanda ya Juu Kusini. Hata hivyo, sekta ya mifugo Mkoani Lindi imeendelea kukua baada ya Serikali ya Mkoa kukubali kupokea mifugo toka Mikoa mingine yenye ng’ombe wengi na mwamko unaoongezeka wa wakazi wa Mkoa wa Lindi katika kujiletea maendeleo yao kupitia sekta ya mifugo.

HALI YA UCHUMI NA MCHANGO WA SEKTA YA MIFUGO KATIKA UCHUMI WA MKOA

Wananchi wengi wa Mkoa wa Lindi wanategemea kuendesha maisha yao ya kila siku kwa kutegemea shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi. Mifugo hii inachangia kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja, Halmashauri na Mkoa kwa ujumla kama ifuatavyo;

Huboresha afya za wanachi kwa kuwa ndio chanzo kikuu cha uto mwili (protein) inayotokana na ulaji wa nyama, maziwa na mayai.

Usalama wa chakula – Mifugo hutumika kama rasilmali hivyo kunapokuwa na upungufu wa aina zingine za vyakula vya nafaka mifugo huuzwa ili wananchi wanunue hivyo vyakula.

Huchangia pato la Halmashauri husika- Mchango wa mifugo katika Halmashuri unatokana na ushuru wa machinjio, leseni za wafanyabiashara wa nyama, ushuru unaotokana na usafirishaji wa mifugo n.k.

Biashara ya mifugo na mazao huchungia mzunguko wa fedha katika Mkoa. Mfano kwa kipindi cha Julai, 2017 hadi Machi 2018 fedha zilizotokana na bishara ya mifugo katika Halmashauri zote Mkoani Lindi ni zaidi ya shilingi 5,103,759,294.91 za kitanzania.

IDADI YA MIFUGO

Mkoa wa Lindi hadi kufikia mwezi Machi, 2018 una jumla ya Ng’ombe wa asili 118,760, Mbuzi asili 79,183, Mbuzi wa kisasa 8,138, na Kondoo 9,007. Mifugo mingine ni Ngamia 10, Nguruwe 5,166, Mbwa 14,488, Kuku 1,460,491, Punda 121, Kanga 5,788, Bata 25,111, Bata mzingi 112, Paka 7,627, Njiwa 1,586 na Sungura 212. Jedwali lifuatalo linaonesha hali halisi ya ukuaji wa sekta ya Mifugo Mkoani Lindi tangu mwaka 2003/04 hadi mwaka 2017/18

 Ukuaji wa Sekta ya Mifugo Mkoani Lindi

Mwaka
2003/04
2012/13
2017/18
Ng'ombe
12,000
40,461
118,760
Mbuzi
34,500
76,088
87,321
Kondoo
12,900
12,742
8,736
Nguruwe
2,400
5,221
5,166
Mbwa
11,280
15,593
14,488
Kuku
16,890
1,700,576
1,460,491
Punda
-
108
121
Bata
3,760
94,962
25,223
Paka
2,670
5,673
7,627
Sungura
-
110
212
Ngamia
-
-
10
Njiwa
200
760
1,586

UENDELEZAJI WA MIUNDO MBINU YA MIFUGO 

Eneo lililotengwa kwa ajili ya malisho.

Halmashuri za Wilaya za Nachingwea, Kilwa, Liwale na Lindi zilikwishatenga maeneo ya kupokea wafugaji kutoka mikoa mingine. Ni Vijiji 59 ambavyo vimeshawekewa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi na kutenga maeneo kwa ajili ya malisho ya mifugo. Maeneo yote yaliyotengwa yana  jumla ya hekta 293,909.69 yenye uwezo wa kutoa malisho kwa idadi ya mifugo ipatayo 146,955.Halmmashauri za Mkoa Lindi zinaendelea na  zoezi la kutenga zaidi maeneo mengine kwa ajili ya kupokea mifugo pamoja na kuimarisha miundo mbinu katika maeneo hayo.

Aidha, katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa hakuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wafugaji lakini kuna mifugo inayotegemea malisho ipatayo 13,589 na 16,529 kwa mfuatano huo.

Malambo/Mabwawa ya maji kwa ajili ya mifugo

Jumla ya malambo na mabwawa yaliyopo katika Mkoa ni 13 ambapo kati ya hayo yanayofanya kazi ni 6, mabovu/yaliyojaa tope ambayo yanayohitaji kufanyiwa ukarabati ni 6 na moja halifanyi kazi.

Majosho

Mkoa una jumla ya majosho 19 ambapo majosho yanayofanya kazi ni 6, majosho mazima yasiyofanya kazi ni 2, mabovu yanayohitaji ukarabati ni 10, na josho moja ni binafsi. Aidha, majosho mengi yameshazungukwa na makazi ya watu hivyo hayafai kutumika kwa mfano katika halmashauri ya Nachingwea.

Mashamba ya Mifugo yaliyopo Mkoani Lindi

Katika Mkoa wa Lindi yapo mashamba 7 ya mifugo ambapo shamba la Mtanga linamilikiwa na Jeshi la Magereza lipo Wilaya ya Kilwa na linafanya kazi, Shamba la Narunyu linamilikiwa na Narunyu Sister’s Convent lipo Wilaya ya Lindi na linafanya kazi, Shamba la Magereza Kingurungundwa linalomilikiwa na Jeshi la Magereza lipo vizuri na linafanya kazi, Shamba la Mayola linalomilikiwa na Ally Mayola lipo Manispaa ya Lindi na Linafanya kazi na Shamba la L.M.U. Farm III linalomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea ambapo uzalishaji wake ni mdogo hivyo linahitaji uwekezaji mkubwa na shamba moja la mfugaji Mkubwa katika kijiji cha Matekwe Halmashauri ya Nachingwea.

Idadi ya minada iliyopo na inayofanya kazi 

Mkoa wa Lindi una jumla ya minada minne (4) kati ya hiyo, miwili inapatikana Kilwa, Manispaa ya Lindi ina mnada mmoja ambao haufanyi kazi na Halmashauri ya Lindi ina mnada mmoja uliokuwa unafanya kazi. Aidha, katika Halmashauri za Liwale, Nachingwea na Ruangwa hakuna minada na juhudi zinafanyika ili kuwa na minada katika Halmashauri hizo.

 Kituo cha uhamilishaji kinavyofanya kazi. 

Katika juhudi za kuendeleza shughuli za uhimilishaji nchini, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imeanzisha kituo cha uhimilishaji cha kanda ya kusini kilichopo Mkoani Lindi. Kituo hiki kipo ndani ya eneo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi na kilifunguliwa rasmi Oktoba 2012. Pamoja na shughuli nyingine kituo hiki kimesimikwa Mtambo wa kuzalisha kimiminika cha hewa baridi ya Naitrojeni ambayo hewa hii hutumika kama pembejeo muhimu ya kuhifadhi mbegu za madume bora na chanjo.

Wizara imejenga kituo hiki ili kukidhi mahitaji ya pembejeo hiyo muhimu kwa wataalamu na wadau wengine wanaofanya shughuli ya uhimilishaji na chanjo kwa wafugaji wanaoishi kwenye mikoa ya kanda ya kusini hususani Lindi, Mtwara na Ruvuma, hivyo kuwapunguzia wataalamu wa uhimilishaji mzigo wa gharama ya kusafiri umbali mrefu kufuata kimiminika hiki muhimu cha naitrojeni cha kuhifadhia mbegu na chanjo Kibaha Mkoani Pwani. Hadi mwezi Machi, 2018 jumla ya ng’ombe 112 wamehimilishwa na ng’ombe wengine 110 wanategemewa kuhimilishwa kuanzia mwezi wa Aprili, 2018

Huduma Zitolewazo na kituo

Kuzalisha hewa baridi ya kimiminika cha naitrojeni na kuuza kwa Taasisi na sekta binafsi.

Kuuza Mbegu za madume bora kutoka Kituo cha Taifa cha uhimilishaji kilichopo Usa River, Arusha (NAIC)-Mbegu bora za ngombe wa maziwa na nyama.

Kuuza Vitendea Kazi vya uhimilishaji.

Kusimamia, kufuatilia na Kutoa taarifa ya uhimilishaji Wizarani na Kituo cha taifa cha uhimilishaji kutoka Mikoa ya Lindi na Mtwara.

MAGONJWA YANAYOSUMBUA MIFUGO

Kuna magonjwa mengi yanayosumbua mifugo Mkoani Lindi kulingana na aina ya mifugo. Kwa upande wa ng’ombe kuna magonjwa makubwa matatu ambayo yanasababisha vifo kwa wingi. Kwanza, ugonjwa wa mapafu (CBPP), Ndorobo (Trypanosomiasis) na minyoo (Helminthosis). Kwa upande wa kuku ni Kideri, Kuhara damu (Coccidiosis), Minyoo na Fowl typhoid (Homa ya matumbo).

Mbuzi na kondoo wanasumbuliwa sana na Kuharisha (Enteritis) na Minyoo (Helminthosis). Kwa miaka mingi magonjwa haya hayakuwepo kutokana na kutoingizwa kwa mifugo kulikosababishwa na hali ya kijografia hasa kuwepo kwa mto Rufiji upande wa kaskazini, mto Lemusule upande wa Magharibi, mto Ruvuma upande wa kusini na bahari ya Hindi upande wa mashariki, hivyo ilikuwa vigumu kwa wafugaji kuingiza mifugo kwa wingi.

Hivyo, Mikoa ya Lindi na Mtwara ikawa ni ukanda huru wa magonjwa ya mifugo (Animal Disease Free Zone), lakini baada ya kukamilika kwa barabara ya Kibiti – Mingoyo kwa kiwango cha lami na ujenzi wa daraja la Mkapa katika mto Rufiji uingiaji wa mifugo umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana na hivyo kuleta magonjwa ambayo hayakuwepo awali.

Hali ya madawa na usambazaji wake.

Hali ya madawa ya mifugo Mkoani Lindi si yakuridhisha kutokana na historia ya mkoa kuwa si wa wafugaji, hivyo kuna maduka machache sana ya pembejeo na madawa za mifugo. Mengi ya maduka haya yapo Manispaa ya Lindi ambako yapo maduka matano tu na kila halmashauri kuna duka moja moja, hivyo, kuna fursa kubwa ya biashara ya madawa ya mifugo na pembejeo zake.

MAZIWA NA MAYAI YALIYOZALISHWA NA THAMANI YAKE

Katika Mkoa wa Lindi maziwa yanayozalishwa kwa siku ni lita 11,389 ambapo lita moja hununuliwa kwa bei ya shilingi 1000 - 2000. Kwa upande wa mayai huzalishwa wastani wa mayaai 7,300 kwa siku ambapo yai moja huuzwa kwa wastani wa shilingi 400 hadi 500. Asilimia 95 ya mayai hutokana na kuku wa asili na kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa mayai hutegemea sana toka Mikoa ya Pwani na Dar -es -Salaam, hivyo ipo fursa kubwa ya uwekezaji hususani katika ufugaji wa kuku wa mayai.

Ufugaji wa kuku na uzalishaji wa mayai

Mkoa wa Lindi una fursa kubwa ya kuwazalisha kuku wengi kwa ajili ya biashara na kuboresha afya ya wananchi kupitia nyama yake na mayai. Hadi sasa hakuna wazalishaji wakubwa wa kuku wa mayai, wafugaji walipo ni wadogo ambao hufuga kuku wasiozidi 20 hasa wa kienyeji. Kutokuwepo kwa wazalishaji wa mayai kumepelekea bei ya trei moja la mayai kuuzwa kwa shilingi 11,000 kwa yale ya kisasa na shilingi 15,000 kwa mayai ya kienyeji.

Aidha, mwezi Februari, 2018 Ofisi ya Mkuu wa mkoa ilipokea barua toka Wizara ya Mifugo na uvuvi ikitambulisha mradi wa uzalishaji wa kuku hususani aina ya Kuroiller unaofadhiliwa na Bill and Melinda Gates Foundation kwa kipindi cha miaka minne kuanzia januari 2018 hadi Januari 2021 na kutekelezwa na Kampuni ya AKM Glitters Ltd ya Dar es Salaam . Aidha, Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri wamejulishwa kuhusu mradi huu na taarifa hizi tayari zilishawafikia wananchi.

Hadi kufika tarehe 31 Machi, 2018 mawakala wawili walipatikana na kuletewa vifaranga vya siku moja 1737 pamoja na vyombo vya chakula, maji na mchanjo. Huduma ya ugani imetolewa ipasavya na Mgani wa Kampuni AKM Glitters. Mawakala wengine watatu wameletewa vifaranga 5940 mwezi Aprili na Mei, 2018. Jumla ya vifaranga vya Kuroiller walioingizwa mkoani Lindi kwa miezi mitatu tangu mradi huu umeanza ni 7677.

Ni matumaini ya Mkoa kuwa mara baada ya halmashauri zetu kuwahamasisha wananchi ufugaji wa kuku utakuwa mkubwa hususan aina hii ya Kuroiller ambao hutaga mayai kuanzia 150 hadi 200 kwa mwaka ukilinganisha na kuku wa kienyeji wanaotaga mayai 40 hadi 50 kwa mwaka. Aidha, aina hii ya kuku hukua haraka na madume hufikia uzito wa kilo 3.5 na majike kilo 2.5 hivyo wataongeza upatikanaji wa mayai na nyama ya kuku na kuweza kuboresha afya ya wananchi.

                    Kuroiller                                   Kuroiller wakiwa Mtanda, Lindi Manispaa

Ulaji wa mazao yatokanayo na mifugo. 

Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa, wastani wa taifa wa ulaji nyama kwa mtu mmoja kwa mwaka ni kilo 12 lakini kwa Mkoa wa Lindi ni kilo 1.5. Kwa upande wa unywaji wa maziwa, wastani wa taifa ni lita 24.6 kwa mtu kwa mwaka wakati Mkoani Lindi ni lita 1.6 tu (tofauti ya lita takribani 23). Vilevile, takwimu zilizopo za ulaji wa mayai kitaifa ni mayai 26 kwa mtu kwa mwaka wakati kwa Mkoa wa Lindi ni wastani wa mayai 13. Katika uzani wa kimataifa, takwimu zilizopo zinaonesha kuwa ulaji wetu kitaifa uko chini ya ule wa Africa

VIWANDA VYA KUSINDIKA MAZIWA

Mkoa wa Lindi hakuna viwanda vya kusindika maziwa badala yake kuna wasindikaji wadogo 5 wanaojihusisha na usindikaji wa maziwa Lindi mjini na shirika la masister wa Narunyu katika halmashauri ya Lindi kwa kiwango kidogo ambacho hakikidhi mahitaji.

IKAMA YA WATUMISHI WA SEKTA YA MIFUGO

Mkoa wa Lindi una jumla ya watumishi wa mifugo 113 wakati mahitaji ni watumishi 262 hivyo upungufu ni watumishi 148. Mkoa utaendelea kuajri watumishi ili kujaza nafasi kadri utakapopata vibali.

HUDUMA NYINGINE ZILIZOTOLEWA NA SEKTA YA MIFUGO

Sekta ya mifugo imekuwa ikitoa huduma mbalimbali zikiwemo za ushauri kwa wafugaji ili wafuge kisasa, Ukaguzi wa nyama zinazochinjwa na machinjio kwa ujumla, shughuli za ugani zimeendelea kutolewa katika ngazi za kata na vijiji na hii ni pamoja na ufuatiliaji wa magonjwa na utoaji wa kinga, kuhasi na upigaji chapa mifugo.

CHANGAMOTO NA MIKAKATI YA KUKABILI

Changamoto

  • Wananchi wengi kuwa na uelewa mdogo wa masuala ya ufugaji
  • Wafugaji kutozingatia kanuni za ufugaji bora
  • Uelewa mdogo juu ya teknolojia ya uhimilishaji
  • Matumizi kidogo ya vyakula vya ziada vinavyotokana na ufuta, korosho, nazi na alizeti
  • Matumizi madogo ya dawa za ruzuku za kuogesha mifugo
  • Ukosefu wa miundombinu na ubovu wa ile iliyopo
  • Zoezi la kupima vijiji kwa ajili ya mipango ya matumizi bora ya ardhi halijakamilika kwa baadhi ya Wilaya.
  • Katika maeneo yaliyopimwa baadhi ya wakulima na wafugaji kutozingatia mipango ya matumizi bora ya ardhi iliyowekwa kwenye maeneo yao
  • Uchache wa minada ya mifugo.
  • Ukosefu wa viwanda vya kusindika mazao ya mifugo kama maziwa, nyama na ngozi
  • Uchache wa miundombinu ya mifugo ikilinganishwa na idadi kubwa ya mifugo inayoingia Mkoani

Mikakati iliyopo

  • Kuhamasisha Halmashauri kutoa elimu ya ufugaji bora wa mifugo kwa wananchi wote
  • Halmashauri kuhamasisha wafanya biashara kufungua maduka yaa vyakula vya mifugo
  • Kuhamasisha Halmashauri kujenga na kukarabati miundombinu ya mifugo kwenye maeneo yao na kuhamasisha wafugaji kuchangia kidogo katika ujenzi wa miundombinu ya mifugo.
  • Kushauri Halmashauri kutenga bajeti kwa ajili ya kukamilisha zoezi la kupima maeneo na kuangalia maeneo mapya ya kutenga kwa ajili ya wafugaji
  • Kuzishauri Halmashauri kusimamia matumizi ya sheria ndogo kwenye maeneo yote yaliyopimwa na yenye mipango ya matumizi bora ya ardhi
  • Kuzishauri Halmashauri kusimamia ipasavyo zoezi la uingiaji wa mifugo kutoka nje ya Mkoa/Wilaya kuhakikisha mifugo inapelekwa kwenye maeneo yaliyokusudiwa tu.
  • Kuhamasisha Halmashauri ziwe na mashamba darasa ya malisho ili wafugaji wajifunze.
  • Kila Halmashauri ihamasishe wadau wa mifugo kuhusu matumizi ya minada na kueneza matangazo         ya minada yao kwa wadau ndani na nje ya maeneo yao.
  • Kuhamasisha Halmashauri kutoa elimu ya namna ya kuboresha masoko ya mazao ya mifugo.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.