RAS LINDI: MFUMO WA GoTHOMIS NI LAZIMA KATIKA VITUO VYA AFYA
Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omary, amewataka watumishi wa sekta ya afya kutumia mifumo ya kielektroniki, hususan mfumo wa GoTHOMIS, ambao ni nguzo muhimu katika kusimamia taarifa za wagonjwa, ukusanyaji wa mapato na utoaji wa huduma bora katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Ametoa agizo hilo katika kikao cha uwasilishaji wa ripoti ya ukaguzi wa Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati wilayani Kilwa, kilichofanyika leo tarehe 14 Novemba 2025.
Aidha, amewaagiza Waganga Wafawidhi wa vituo hivyo kuhakikisha wanawashirikisha watumishi wenzao katika kujadili changamoto zinazowakabili ili kuwe na utatuzi na uwajibikaji wa pamoja. Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dkt. Kheri kagya ametoa wito kwa watumishi hao kuzingatia maadili ya taaluma yao Aidha, amehimiza kuwepo kwa mpango maalumu wa kuboresha huduma kwa wagonjwa ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya Naye, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilwa, Ndg. Yusuf Mwinyi, amewataka watumishi wa sekta hizo kuwajibika ipasavyo, akisisitiza kuwa ukaguzi unaweza kufanyika wakati wowote ili kuhakikisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Kadhalika Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Ndg. Hemed Magaro, pamoja na waganga wafawidhi wa vituo hivyo wameahidi kushughulikia changamoto zinazoikabili sekta ya afya ili kuimarisha ustawi wa sekta hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.




Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.