Mwenyekiti wa kamati ya lishe Mkoa Bi. Zuwena omary ametoa wito kwa wajumbe wa kamati hiyo kuongeza hamasa ya kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa ulaji unaofaa .
Wito huo ameutoa wakati wa mjadala wa namna ya kuendelea kuhakikisha jamii inazingatia kanuni za afya bora kupitia vyakula vyao kwa kuwapa utaratibu nzuri .
"Ninaimani kuwa wananchi wakielekezwa na kuelimishwa mara kwa mara kuhusu chakula bora na mpangilio wake, wanatekeleza , watanzania waaminifu na watiifu sana katika kuzingatia Maelekezo hasa kwa wamama wajawazito " Bi Zuwena omary
Mwenyekiti ametoa eqito huo kufuatia taarifa ya hali ya lishe katika mkoa wa Lindi kwa kipindi cha julai hadi Septemba 2024 kupitia tafiti zilizofanyika kwa baadhi ya viashiria vya hali mbalimbali ikiwemo udumavu waliopimwa zaidi ya Elfu 13, waliobainika na udumavu ni 178 Sawa na 0.1%, hali ya ukondefu waliopimwa zaidi ya elfu 13, waliobainika 133 sawa na 0.1 % na upungufu wa damu kwa wanawake walio katika umri wa uzazi waliopimwa elfu 9 waliobainika 190 sawa na 2.1%
Imebaini uwepo wa kiashiria cha watoto wanaozaliwa na uzito pungufu yaani uzito chini ya 2.5kg , ambapo tatizo ni kubwa kwa halmashauri ya @lindimanispaa Lindi Mc 9.54, @ruangwadc Ruangwa DC 5.25%, @nachingwea_dc Nachingwea DC 5.19%, @mtamadcofficial Mtama DC 5.53, @liwaledc Liwale DC 8.59% halmashauri husika zimetakiwa kuendelea kutoa elimu ya lishe kuhusu ulaji unaofaa wakati wa ujauzito ili kukabiliana na changamoto hiyo.
Licha ya changamoto hiyo bado hamasa ya lishe inaendelea na kufanikiwa katika maeneo kadhaa ambapo kiashiria cha idadi ya wanafunzi wanaopata angalau mlo mmoja wakiwa shuleni kimeendelea kuongezeka ngazi ya mkoa kutoka 73.49% April -Juni , 2024 hadi kufikia 75.43% Julai -Spetemba , 2024
@maendeleoyajamii
@ortamisemi
@jirized
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.