Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Lindi, ikiambatana na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Ndg. Juhudi Mgallah, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Mipango na Uratibu, Kamati hiyo ikiongozwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Lindi, Ndg. Barnabas Essau, imepongeza uongozi na wataalamu wa Wilaya ya Liwale kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo.
Ziara hiyo imeambatana na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Liwale, Mkuu wa Wilaya, Mhe. Goodluck Mlinga, Katibu Tawala wa Wilaya, Bi. Azilongwa Bohari, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya, Bi. Tina Sekambo, pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri.
Pongezi hizo zimetolewa, Februari 11, 2026, wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Liwale. Katika ziara hiyo, kamati imekagua mradi wa maji katika Kijiji cha Turuki wenye thamani ya shilingi bilioni 6.9.
Aidha, kamati imekagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya elimu ya awali na msingi katika eneo la Shule ya Sekondari R.M. Kawawa wenye thamani ya shilingi milioni 314, pamoja na mradi wa ujenzi wa Kituo kipya cha Afya Mbaya wenye thamani ya shilingi milioni 280.
Wakiwa katika mradi wa ujenzi wa shule hiyo, wajumbe wa kamati wamekagua ujenzi wa madarasa sita kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la sita, madarasa mawili ya elimu ya awali, jengo la utawala pamoja na matundu ya vyoo.
Vilevile, katika mradi wa ujenzi wa Kituo kipya cha Afya Mbaya, kamati imekagua ujenzi wa jengo la maabara na jengo la wagonjwa wa nje (OPD).






Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.