• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mkoa wa lindi

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa Mkoa wa lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

KAMATI YA SIASA YAKAGUA NA KURIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM WILAYANI KILWA

Posted on: February 12th, 2026

Leo, Februari 12, 2026, Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Lindi imeendelea na ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Kilwa, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inatekelezwa ipasavyo wilayani humo.


Ziara hiyo iliongozwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Lindi, Ndg. Barnabas Y. Essau, akiambatana na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ndg. Juhudi Mgallah ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Mipango na Uratibu, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Mohamed Nyundo, wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa na Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Ndg. Hemedi Magaro, pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri.


Baada ya kukagua miradi mbalimbali, Kamati imeridhishwa na kiwango cha utekelezaji na kupongeza juhudi zinazofanywa na uongozi wa Wilaya katika kusimamia miradi hiyo, kwa kuzingatia maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Akizungumza mara baada ya ukaguzi, Ndg. Essau amesema:

“Tumekagua miradi na kujionea utekelezaji wake. Miradi ni mizuri na inatekelezwa kwa kiwango cha kuridhisha. Nawapongeza viongozi wa Wilaya, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri, kwa kazi nzuri mnayoifanya. Hongereni sana wanakilwa.”


Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa Ghala la Kuhifadhia Mazao la Halmashauri, ujenzi wa Daraja la Somanga, ujenzi wa Soko la Wafanyabiashara Wadogo katika Kijiji cha Njia Nne, pamoja na ujenzi wa Stendi ya Nangurukuru.


Kwa upande wake, Ndg. Mgallah ameupongeza uongozi wa Wilaya kwa hatua kubwa za maendeleo zilizofikiwa, akieleza kuwa maboresho yaliyofanyika yameleta mabadiliko chanya na taswira mpya ya maendeleo katika eneo hilo.


Ziara hiyo ni sehemu ya tathmini ya mara kwa mara ya miradi ya maendeleo inayolenga kuimarisha uwazi na uwajibikaji, kuongeza kasi ya utekelezaji, na kuhakikisha miradi inaleta manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi wa Wilaya ya Kilwa.





Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • LINDI MANISPAA YANG'ARA KWA UFANISI UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM

    February 13, 2026
  • KAMATI YA SIASA YAKAGUA NA KURIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM WILAYANI KILWA

    February 12, 2026
  • MIRADI YA BILIONI 7.6 YATEMBELEWA WILAYANI LIWALE NA KAMATI YA SIASA MKOA WA LINDI, YATOA PONGEZI KWA UTEKELEZAJI

    February 11, 2026
  • Picha za matukio mbalimbali wakati wa ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyofanywa na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Lindi katika Wilaya ya Nachingwea.

    February 11, 2026
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.