• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

MAWASILIANO YA BARABARA SOMANGA -MTAMA YAANZA KUREJEA , ABIRIA WAPONGEZA JUHUDI ZA SERIKALI

Posted on: April 8th, 2025

Mawasiliano ya Barabara Somanga - Mtama yameanza kurejea kwa hatua katika barabara iendayo mikoa ya Kusini tangu leo alfajiri  baada ya wataalamu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) kufanya kazi usiku na mchana kurekebisha eneo la Somanga na Matandu lililoharibiwa na mvua na kufanya njia isipitike.

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ambaye ameweka kambi katika eneo hilo tangu jana, amewaambia waandishi wa habari kwamba magari madogo 230, mabasi 10 na baadhi ya malori 30 yaliyobeba bidhaa mbalimbali ikiwemo mawe makubwa yamefanikiwa kuruhusiwa kupita katika eneo la Somanga Mtama na Matandu kuanzia leo kati ya saa 11:30 alfajiri hadi saa 12:00 asubuhi.

Ulega ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa ya awali akiwa mkoani Lindi wakati akiendelea kusimamia zoezi la urejeshaji wa maeneo yaliyokatika katika barabara kuu ya Dar es Salaam - Lindi linaofanywa na Timu ya  Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara (TANROADS) kwa kushirikiana na Mkandarasi.

Baadhi ya abiria waliolazimika kusubiri usafiri usiku kucha wamezungumza na waandishi wa habari na kutoa shukrani kwa wataalamu waliofanikisha kazi hiyo kwa kufanya kazi usiku kucha.


“Tunaishukuru sana serikali hasa wataalamu wake na mheshimiwa Waziri wa Ujenzi ambaye tumeshinda naye hapa kutwa nzima mpaka jioni na akatuahidi leo tutaondoka na neno lake limetimia,” alisema Shaaban Matwanga mkazi wa Lindi ambaye ameondoka kwenda Dar es Salaam leo.

Katika maelezo yake, Ulega alisema matengenezo zaidi katika maeneo ya Somanga Mtama na Matandu yanaendelea kuimarishwa kwa kuendelea kuwekwa mawe makubwa ili kuruhusu na magari mengine yaliyobakia kupita.

Ulega amewahakikishia Watanzania kuwa serikali ipo kazini usiku na mchana katika kuhakikisha miundombinu ya barabara hiyo inaimarishwa ili isiwe kikwazo kwa wasafiri.

@wizara_ya_ujenzi

@zainabutelacky

@ikulu_mawasiliano

@gersonmsigwa

@nchikwanza

@ortamisemi

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.